2018-04-28 14:14:00

Tume ya Kitaifa ya Kiekumene imetoa wito kwa nchi ya Pakistani kulinda amani


Kuhukumu kutumia nguvu hasa katika mashambulizi yanayozidi kurudiwa dhidi ya wakristo huko Quetta na Lahore, ndiyo wito kwa Serikali ya Pakistani ili kweli wahalifu waweze kutendewa haki yao. Ndiyo utashi na mapendekezo yaliyo wakilishwa na washiriki wa mkutano, ulio andaliwa huko Lahore na tume ya kitaifa ya Baraza la Kiekumene na mazungumzo ya kidini ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Pakistan, kwa kushirikiana na Chama cha Mungano wa dini (Uri). Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuonesha mapenzi ya wakristo na waislam kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani na umoja, ambapo mkutano huo umeweza kugusa zaidi juu ya matendo ya vurugu ya nguvu ambayo yamekumba nchi ya Pakistan.

Mnamo tarehe 15 Aprili kama inavyojulikana  katika mtaa wa wakrsto  huko Essa Nagri, mjini Quetta, mji mkuu wa Baluchistan, kulitokea mashambulizi ya kigaidi na kusasababisha wakristo wawili , wakiwa mkatoliki na mluteri mmoja na wengine watano kufariki dunia. Na katika siku hiyo hiyo pia katika kanisa la  kiinjili kwenye mji wa Shahdara  huko Lahora, lilichomwa moto. Matukio hayo yametoa wasiwasi mkubwa , hadi kufikia tume ya kitaifa ya haki na amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki kuandaa hata maandamano katika nchi nzima ili kupinga na kuonesha mshikamano kwa wakristo wa Quetta na Lahore na ili kuhamasisha Taasisi za kisiasa na haki zijikite barabara katika kuthibiti hali mbaya isiendelee.

Kwa mantiki hiyo katika mkutano wao wa mazungumzo ya kidini, wameweza kutoa hoja kwamba, kuna haja ya uwajibikaji katika kuhakikisha usalama kwa kila mzalendo bila ubaguzi pia wanataka usalama katika nyumba zao, makanisa na mashuleni. Serikali ya Pakistani inapaswa kuchukua hatua za kisheria katika usalama ili kuwahakikishia hata wakristo usalama wao kwa mujibu wa katibu mtendaji wa Tume ya  kiekumene na mazungumzo ya kidini Padre Francis Nadeem.

Na kwa mujibu wa kiongozi mkuu  wa kiislamu nchini humo, amesisitiza kwamba, wanapaswa kuonesha ujasiri na shauku ya kufanya kazi ya mipango ya pamoja, kuhamasisha amani na kupinga dhidi ya ugaidi, aidha, wakristo na waislam ni ndugu ambao daima wanapaswa kutembea pamoja na kutoa mchango na uelewano katika imani zao.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.