2018-04-28 14:27:00

Kushiriki na Mungu kwa njia ya Utatu inatuwezesha kufikia wokovu !


Katika Barua ya“Placuit Deo” ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki, inayohusu  baadhi ya mantiki ya wokovu wa kikristo, iliyotangazwa  tarehe 1 Machi 2018 ikiwa imeidhinishwa na Papa Francisko na saini ya Askofu Mkuu, Luis Francisco Ladaria Ferrer, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Askofu Mkuu Giacomo Morandi, Katibu wa Baraza hilo, inaonesha jinsi gani siri ya mapenzi ya Mungu tumeirithi kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo.  Maana ni kwa njia ya Yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Umungu, mkikombolewa kutoka uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Na ili tupate na urithi usio haribika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. (taz Ef 19); Pt 1,4). [...].

Waraka huo unaendelea kufafanua zaidi ya kwamba: Katika karne ya XIX, mwana falsafa na Mtaalimungu wa Urusi Vladimir Solovyov (1853-1900) aliweza kutoa mchango mkubwa katika masuala na maana ya taalimungu. Lakini Solovyov hakufanya hivyo kwa sababu ya taalimungu ya kiorthodox, bali hata mawazo ya Kanisa la Ulimwengu. Katika maandishi yake mnamo mwaka 1886 aliweza kuonesha  bayana juu ya uhusiano ya Ukristo na Israeli. Solovyov aliona kuwa, uhusiano huo  pamoja na kuwa na ndiyo uzao wa Yesu lakini ulikuwa pia ni msingi wa taalimungu! Enzi hizo wazo la utakatifu wa mwili na dukuduku za mawazo haya ya maisha ya Israeli yalichangamotisha sana, hasa kwa kutaka kuona umuhimu wa kila mtu kwa sababu katika sehemu kubwa  ya historia ya maandiko matakatifu yalijikita katika sheria ya Musa! 

Lakini kwasasa, iwapo kuna kukabiliana na  matashi ya wayahudi katika  hali halisi, misingi  ya Mungu na shughuli za kujitakasa na kutakatifuza miili ya watu, inawezakana kabisa kutambua kwa urahisi mazingira ya wayahudi zaidi kwa kupitia muungano wa  “Neno kufanyika mwili”. Tunaweza kutambua ukuu wa kihistoria na kuuchukulia kama ufunguo Waraka wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika mantiki ya  wokovu wa kikristo kwa sababu ya mwili, nyenzo  na roho. Kwa maana hiyo mtaalimungu Solovyov alitoa utangulizi wa maneno ambayo kwa namna nyingine ni sehemu ya maneno ya Kristo mwokozi wa ulimwengu, wakati wa mahubiri yake. Pamoja na hayo, hata leo hii bado zinaendelea mijadala mingi, hata  tabia na mantiki za kisasa, vile vile  kwa ufafanuzi tena wa  mfano wa waraka wa  kwanza  uliotolewa moja kwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika tamko la “Dominus Iesus 2000” kuhusu "umoja na wokovu wa dunia wa Yesu Kristo na Kanisa lake" (wakati ule  Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  alikuwa ni Kardinali Joseph Ratzinger na katibu wake Askofu Mkuu Tarcisio Bertone, S.D.B.)

Kutokana na hiyo, Waraka wa Placuit Deo, wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa mwaka uliotolewa tarehe 1 Machi 2018, unaonesha tabia mbili ambazo zinajaribu kufafanua juu mawingu mawili  meusi, ili kuweza kupta utambuzi wa kikristo kama wokovu unatoka moja kwa moja kwa Mungu na kuufikia ulimwengu. Tabia za mawingi meusi yakutokana na  kwamba, tangu hawali kumekuwa na uzoefu wa kupinga mafundisho msingi ya Kanisa  hasa juu ya ukombozi na dhana ya kuweza kujisafisha dhambi ya mauti na ugnostiki katika Kanisa, yaani kutafuta ukombozi binafsi.

Kwa kufafanua,zaidi kipengele cha kumi kinaonesha kuwa, ni wazi kuona kwamba wokovu ambao Yesu ameuleta yeye mwenyewe hautokani na mawazo yake binafsi, bali kwa ajili ya kutangaza kwa kila mmoja, juu ya  muungano wa wokovu na Mungu ulivyotokana na Mwanae kujifanya mtu (Yh 1,14), na kutwaa mwili (taz. Rm 8, 3; Eb 2,14; 1 Yh 4,2), akazaliwa na mwanamke (taz. Gal 4, 4) ambaye ni mwana wa Mungu, ambaye ni mwana wa binadamu na ndugu yetu (taz. Eb 2,14). Kwa njia ya kujifanya sehemu ya familia ya binadamu, ameungana kwa namna moja na kila binadamu na kufanya mahusiano na Mungu, Baba yake na watu wote mahali ambapo wote tunaweza kushiriki maisha yake mwenyewe. Matokeo ya kuja kwake, ambayo yaletayo wokovu katika Kristo, yamewezesha wana wa Adamu  kupata wokovu kutoka kwa Mungu. 

Hatimaye katika kujibu zile aina mbili za kupinga dini  kwa dhana binafsi, ndani ya Kanisa na ile ya unyostiki ambao unaruhusu uhuru wa ndani, ni lazima kukumbush ajinsi gani Yesu ni Mwokozi. Tabia ya unyostiki inakuwa na  kikwazo cha kuonesha njia ya kuweza kukutana na Mungu, wakati huo hu ni njia ambayo tunaweza kuikimbilia kila mmoja hasa kwa kupitia njia ya  kufuata maneno na mifano ya Yesu Kristo. Na Zaidi, ili Kristo aweza kufungua milango ya ukombozi, yeye mwenyewe anageuka kuwa njia kwa maana anaelekeza “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”(taz. Yh 14,6).  Pamoja na mchakato wa njia hiyo lakini haukumfanya havunje mahusiano ya ndani na wengine na kazi ya uumbaji. Kinyume chake Yesu alitupatia njia mpya hai  ambayo yeye mwenyewe alianzisha tangu alipochukuliwa mwili, maana,“njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake”  (taz Eb 10,20). Kutokana na ufafanuzi huo unatoa ushuhuda wazi ya kuwa Yesu ni Mwokozi kamili, maana alichukua ubinadamu wetu kamili na kuishi kama binadamu kamili katika muungano na Baba na ndugu. Wokovu wake unatokana na njia hiyo ya kutwaliwa maisha yake hayo ndani  ya umbu la binadamu na kama asemavyo Mtakatifu Yohane kuwa: “Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake”(taz.  1 Yh 4,13). Yeye tangu mwanzo alikuwa hivyo na kwa maana hiyo amaetupatia kila neema kwa mujibu wa binadamu. Yeye asili yake ndivyo alivyo lakini wakati huo huo ni Mkombozi na mwakozi!

Kipengele cha 12 cha Waraka wa Placuit Deo, kinaendelea kufafanua kwamba, sehemu ambayo tunapokea wokovu uletwao na Yesu ni Kanisa, kwa maana ya jumuiya ya wale ambao pamoja na kuunganika katika mpango mpya wa mahusiano yaletwayo na Kristo, wanaweza kupokea kwa ukamilifu wa Roho wa Kristo,hata barua ya Mtakatifu Paulo kwa Waroma, “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake” ( taz. Rm 8,9). Kutambua vema ngazi hiyo ya Wokovu wa Kanisa, ni msaada muhimu kwa ajili ya kushinda kila aina ya tabia za kupunguza ukuu huo. Wokovu wa Mungu unatusaidia, lakini ambao haupatikani kwa njia ya nguvu zetu binafsi kama ile tabia ya mawazo ya kizamani ya wapinga dini, kinyume chake ni kwa njia ya mahusiano ya dhati ambayo yanatokana na Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu na ambaye anaunda muungano kamili na Kanisa.

Pamoja na hayo, neema ya Kristo ambayo inatolewa, tofauti na zile mbizi za wapinga dini wenye kutaka kujitafutia  wokovu wa ndani tu bila kujibidisha katika hatua ya uongofu wa kweli,  ni ile ya kuunda mahusiano ya kweli ambayo Yesu mwenyewe aliishi kwa maana ndani ya  Kanisa ni Jumuia inayoonekana. Na Kanisa linagusa mwili wa Yesu kwa namna ya pekee kupitia matendo hai ya maskini na wote wanaoteseka. Katika kuelezea kwa ufasaha zaidi daraja la wokovu wa Kanisa. Sakramenti ya  wokovu wa  ulimwengu inatuhakikishia kwa kina zaidi ya kwamba, wokovu hautokani na njia ya kujitosheleza binafsi kwa kutafuta uongofu wa ndani katika Mungu tu,kinyume chake ni kutufundisha kwamba, ni lazima kushiriki kwa dhati muungano wa Mungu na mtu ambaye anashiriki kikimalifu katika muungano na Utatu Mtakatifu!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.