2018-04-26 16:30:00

Tanzania yaadhimisha miaka 54 ya Muungano


Tanzania inaadhimisha miaka 54 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda taifa moja la Tanzania. Ilikuwa tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika iliungana na Zanzibar na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maadhimisho ya mwaka huu yameyongozwa na rais John Pombe Magufuli mjini Dodoma, na yamefanyika wakati muungano huo unaendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali za kijamii na kisiasa.

Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya habari mahalia vinasema kuwa, Rais John Magufuli, ameupandisha hadhi Mkoa wa Dodoma kuwa Jiji kuanzia leo Aprili 26 huku akisisitiza azma yake ya kuhamia jijini humo iko pale pale. Uamuzi huo ameutangaza wakati akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho miaka 54 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma. Kadhalika amesemakuwa kunzia leo kwa mamlaka waliyompatia Watanzania Dodoma ni Jiji na Mkurugenzi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa sasa anakuwa Mkurugenzi  wa jiji.  Pamoja na mambo mengine wakati wa hotuba yake  amesema, Dodoma iko katikati ya Tanzania ambapo sasa ile miradi iliyoombwa na serikali kwa Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), wajue haiendi manispaa bali inakwenda kwenye jiji.

Tukirudi katika changamoto inayoikumba Tanzania kwa sasa ni ile iliyojitokeza hivi karibuni kutokana  na mitandao ya kijamii kwa mfano, mwanaharakati katika mitandao ya kijamii, mtanzania ambaye anaishi nchini Marekani kwa jina Mange Kimambi, amekuwa akiratibu maandamano kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiitisha maandamano nchi nzima dhidi ya rais John Magufuli kwa kile anachodai kuwa amekuwa akikiuka haki za binaadamu na kukandamiza uhuru wa kisiasa nchini Tanzania.

Hata hivyo kupitia vyombo vya habari mahali, Rais Magufuli alipiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa tangu alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi, na hiyo kwa lengo kuu makusudi hasa akitamka ya kwamba uchaguzi umekwisha sasa ni wakati wa kuchapa kazi. Na ndiyo moto wake wa  kampeni ya uchaguzi yaani “Hapa ni kazi tu”.

Katika vyombo vya habari na clip mbalimbali za hivi karibuni zilizotolewa kwenye mitandao, polisi walithibitisha na kuhaidi adhabu kali kwa wale ambao wangejaribu kuitikia wito wa kuandamana dhidi ya serikali. Vile vile kulingana na tamko mbalimbali la kutoa  onyo hilo la polisi wa Tanzania nchini Marekani na Uingereza wametoa wito kwa raia wao waishio nchini Tanzania kuwa waangalifu.

Ni wakati wa kutafakari kipi kinapaswa kutekelezwa katika nchi yenye utajiri na kujulikana katika kulinda amani ya nchi na dunia nzima.
Kwa msaada wa waasisi wa nchi ya Tanzania, watu wake wanaweza kujifunza kutokana na utamaduni wao, mila na desturi za kulinda amani na hasa katika kutunza heshima na kuheshimiana  badala ya kuiga tamaduni za wengine ambao kwa mihongo mingi wameendeleza maandamano , lakini ambayo matokeo yake ni ghasia na kukosesha amani na utulivu wa walio wadogo na wadhaifu.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.