2018-04-20 16:30:00

Papa: Mtumishi wa Mungu Don Tonino Bello ni mfuasi wa Kanisa linaloka nje


Tarehe 20 Aprili 2018 Baba Mtakatifu, Francisko amefanya ziara ya kitume huko Alessano -Lecce, katika Jimbo la Ugento- Santa Maria wa Leuca na  huko Bari katika  jimbo la Molfetta- Ruvo-Giovinazzo-Terlizzi, katika tukio la miaka 25 tangu  kifo cha mtumishi wa Mungu askofu Tonino Bello kilichotukia tarehe 20 Aprili 1993.

Saa moja asubuhi ya tarehe 20 Aprili, Baba Mtakatifu Francisko ameacha Vatican kuelekea mkoa wa Puglia mahali ambapo kwanza amepitia maeneo alikozaliwa  Askofu Tonino Bell, aliyekuwa Asofu wa Jimbo la Molfetta-Ruvo-Giovinazzo-Terlizzi nchini Italia, katika kukumbuka kama mchungaji mwema wa kuigwa  kwa ajili ya watu walio wa mwisho na zaidi mfano wa  mtume wa amani bila kutumia silaha. Ziara yake fupi imetukia  katika madhimisho ya miaka 25 tangu kifo chake Askofu Tonino, kilichotokea Molfetta tarehe 20 Aprili 1993. Kifo chake kilitokana na ugonjwa wa saratani.

Askofu Tonino anafikiriwa kama mfuasi wa Kanisa linalotaka kutoka nje kwa maana ya kuwa maskini kwa ajili ya maskini, jambo ambalo linapendwa sana na Baba Mtakatifu Francisko. Na mnamo tarehe 27 Novemba 2007 Baraza la Kipapa la  kuwatangaza watakatifu watakatifu, lilidhia  mchakato wa kumtangaza  mwenye heri.

Ni karibia masaa manne ya ziara fupi hiyo kati ya maeno ya mkoa wa Puglia, lakini yaliyojaa mambo memngi muhimu. Baba Mtakatifu, mara baada ya kuanza safari na ndege kutoka uwanja wa Champino ametua saa 2.30 asubuhi  huko Alessano, mahali ambapo mara baada ya kufika amekaa kwa kutafakari kwa sala  kwenye kaburi la Mtumishi wa Mungu Askofu Tonino Bello na kuwasalimia ndugu jamaa na marafiki. Baadaye amekutana na waamini na kutoa hotuba yake katika uwanja mkubwa mbali kidogo na Makaburi na kuwasalimia wawakilishi wa waamini kabla ya kuondoka. 

Baada ya kufika katika uwanja wa ndege akitokea Alessano amewasili katika uwanja mkubwa wa Mtakatifu Andrea, karibu na Kanisa Kuu la Molfetta na kupokelewa na Askofu Francesco Cornacchia  wa jimbo Molfetta-Ruvo-Giovinazzo-Terlizzi na Meya wa Mji Dk Thomasi Minervini.

Akiwa katika gari amewasalimia waamini  hata waliokuwa wamekaa katika viti vyao hadi katika jukwaa ambalo limeandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Misa Takatifu. Baada ya Misa Takatifu, Askofu Domenico Cornacchia amemshukuru sana Baba Mtakatifu kwa ujio wake na kuwasalimia wawakilishi wa waamini wa jimbo la Molfetta , amewabariki na baadaye kurudi mjini Vatican. 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News! 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.