Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi, Jumatano tarehe 18 Aprili 2018 ametoa wito wa aina mbili, kwanza kuhusu mkutano wa wahusika wa kifedha dunina kwa ajili ya maskini na wito wa pili kwajili ya kufanya kila iwezekanavyo kutunza maisha hasa wa mtoto Alfie Evans na Vincent Lambert. Baba Mtakatifu akitoa wito juu ya mkutano wa Fedha Marekani, mara baada ya katekesi yake kuhusu Ubatizo amesema kwamba, Jumamosi utafanyika mkutano wa Banki duniani huko Washington na hivyo anawatia moyo katika juhudi za pamoja wahusika wa fedha ili watafute kuhamasha hali ya maisha hasa wale maskini na kuendeleza kwa dhati mendeleo kamili ya heshima ya hadhi ya binadamu!
Wito wa pili ulikuwa unatoa kuwa na umakini wa maisha ya Vincent Lambert na mdogo Alfie Evans. Na kuthibitisha kuwa, mkuu wa maisha tangu kutungwa kwake hadi mwisho wa asili ni Mungu. Ni wajibu wetu kufanya kila iwezekanavyo kutunza maisha. Na kwa ukimya ameomba wote wasali ili maisha yaweze kuhshemiwa kwa kila mtu na zaidi kwa ndugu hao wawili. Amewaalika watu wote ambapo kwa mujibu wa takwimu wanasema walikuwa ni waamini na mahujaji 17,000 katika uwanja wa Mtakatifu Petro.
Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko asubuhi na mapema ya tarehe 18 Aprili 2018 kabla ya kuanza Katekesi yake amekutana na Thomas Evans, baba yake Alfie Evans, taarifa hizo zimeandikwa katika Gazeti la Nuova Bussola Quotidiana:http://www.lanuovabq.it/it
Katika Gazeti la Nuova Quotidiana linaandika kuwa, Tohamas Evan, Baba yake Alfie, amefika asubuhi na mapema mjini Roma, akisndizwa na mwandishi wa Gazeti hilo, Benedetta Frigerio, kukutana kwa faragha na Papa Francisko, na baadaye kuendelea na Katekesi katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Mkutano wa faragha umedumu kwa dakika 20. Makutano hayo kutokana na Askofu Francesco Cavina wa Jimbo la Carpi (MO) nchini Italia, ambapo pia Papa Francisko amemkadhi Askofu huyo, kuendelea na mahusiano kati ya Sekretarieti ya Vatican na wazazi wa mtoto huyo kwenye mchakato wa kuhamisha mtoto huyo katika Hospitali ya Bambin Gesu’ Roma. Katika mkutano na kijana huyo na Papa Francisko kwa lugha ya kingereza amemwambia kwamba,“pambana kwa ajili ya mtoto wako na kwa ujasiri kama Mungu anavyo tetea watoto wake”.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©. |