2018-04-16 16:33:00

Papa amekutana na watoto na wazee wa Parokia ya Mt.Paulo wa Msalaba!


Mara bada ya utangulizi wa Paroko, kumtambulisha juu ya shughuli za kichungaji za Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Msalaba, wakati wa kukutana familia 100 zikiwa zinawakilisha wazee wengine wa Parokia hiyo,   Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba, amekutana na vijana waliokuwa wamejaa wasiwasi na kuuliza maswali, lakinii wazee hao wametulia, hivyo waendelee mbele kwa taratibu kwasababu maisha yamewafundisha  mengi na wanao uzoefe mkubwa! Wengine wanasema vijana wanakimbia lakini, wazee wanafahamu hilo na wanatambua vema njia za maisha ambayo wakati mwingine ni mateso na majaribu, lakini Bwana anawapenda na kile  wanachotenda wanaparokia ni wajibu!

 Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa: wenye kuhitaji, ndiyo msingi wa Parokia na kitovu cha Injili. Ndiyo maana amependa maneno ya paroko wakati wa utangulizi wa hotuba yake fupi, ambapo amesema kuwa, wanafanya kazi kwa ajili ya wazee, hivyo Papa  ana utambuzi wa kila mmoja kuwa na matatizo kama vile  magonjwa, uchungu matatizo ya kiroho, familia na mambo mengine mengi  ambayo wote wanayafahamu. Kila mmoja anao uchungu wake na majeraha yake binafsi. Lakini pamoja na hayo, yasiwaondolee matumaini na furaha kwasababu Yesu amekuja na kulipa majeraha haya katika majeraha yake msalabani. Na ndiyo furaha kwamba, Yesu amelipa kwa ajili ya wote, yuko karibu anawapenda na wafikirie kwamba  mateso hayo tayari yamelipwa juu msalabani na Yesu kwa ajili ya wote!

Akihitimisha amewahimiza waendelee kutenda  wema kwa ajili ya  wengine, kwasababu kila mmoja anao uwezo wa kufanya hivyo, hasa kuanzia katika sala kwa ajili ya wengine. Na ifanywe kwa furaha, yaani furaha ya kuwa mkristo. Ameshukuru ujio wao katika parokia na kwamba wao ni tunu ya Parokia, kama alivyosema Paroko wa Parokia hiyo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.