Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya lapata "vigogo wapya"

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limechagua "vigogo" watakaoliongoza Baraza hili kuanzia sasa! - AP

16/04/2018 11:42

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limefanya mabadiliko katika uongozi wa Baraza kwa kumchagua tena Askofu Philip Arnold Subira Anyolo kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, msimamizi mkuu wa Sekretarieti, msemaji mkuu na mwakilishi mkuu wa Baraza ndani na nje ya Kenya. Askofu John Oballa Owaa wa Jimbo Katoliki la Ngong, Kenya amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais, Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani na pia Mwenyekiti wa Tume ya fedha.

Askofu mkuu Martin Kivuva Musonde ataendelea kuwa ni Mwenyekiti wa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Kenya. Hawa ni baadhi ya viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya waliotangazwa na Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi, hapo tarehe 13 Aprili 2018, mara baada ya mkutano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

16/04/2018 11:42