2018-04-09 15:27:00

Taalimungu Afrika: Utume wa Kanisa la Afrika unatokana na huruma!


Utume wa Kanisa unatokana na huruma, yaani upendo ambao unahisi tasaufi yake katika jamii ya watu. Huruma maana yake ni kuacha uguswe na udhaifu wa watu wengine, ambapo hata katika Biblia, kwenye historia ya kitabu cha Kutoka inaelezea kwa dhati. Ni maelezo yaliyotumwa na Padre Donald Zagore Mtaalimungu wa Chama cha wamisionari wa Afrika katika Gazeti Katoliki la Fides, akihamasisha juu ya uwepo wa huruma  na matendo ya Kanisa katika  ukuu wake katika  hali halisi inayofumbata Bara la Afrika. Padre Zagore anasisitiza kuwa: shughuli mbili msingi zinaeleza tabia ya matendo ya Mung; ya kwanza ni umakini ambao Mungu anajikitia anashiriki mateso ya binadamu.Yeye anaguswa udhaifu wa watu wake mateso ambayo ni uzoefu wa uchungu wa binadamu. 

Pamoja na hayo, lakini Mungu hasimami kamwe na kutazama tu bali anajita katika matendo ya dhati. Yeye mwenyewe anaamka na kwenda kukutana na binadamu ili kumpatia uhuru wa wokovu. Kwa kutazama katika shughuli zote za wokovu wa Kristo kwa binadamu, bado unajikita na kuendelezwa kwa njia ya makuhani. Yeye anabaki kuwa na huruma kwa ajili ya wenye dhambi, maskini,wenye njaa na wote walio fungwa kimwili, kiroho na haya kiutamaduni. Alionesha hivyo kuwa anaguzwa na mateso, umaskini na udhaifu wakati wa akilila kifo cha rafiki yake Lazaro.

Krosto hasimamu kwa urahisi katika mantiki  ya huruma tu yeye binafsi anaamka na kujikita katika maendo ya dhati na kwa maana hiyo, Yeye anaponya wagonjwa, anawapa anawashibisha chakula  umati wa watu, anawafufua katika wafu, anawasamehe dhambi na kuwatangazia habari njema ya ufalme wa Mungu na kuwapa uhuru wote waliofungwa.

Na ndiyo mantiki ambayo inapaswa kutazamwa katika uso wa Kanisa la Afrika ambalo watu wake daima wako mstari wa mble kuwa  karibu na yule anayeteseka na kupeleka Habari njema ya Upendo wa Mungu!  Na katika mantiki hiyo Padre Zgore anasisitiza kuwa, ndiyo msingi wa shughuli zote za kimisionari kwa Kanisa ambalo linafunguka na kwenda kugusa hali halisi ya mateso ya kiroho, kimwili na maadili ya binadamu.
 
Kanisa la Afrika lazima lijikite kwenda katika mipaka yake na  kushinda kila aina ya  vizingiti vingi vitokanavyo na mabadiliko ya hali ya hewa na  utamaduni, ili kuweza kutoa uhuru, amani, na furaha ambayo Injili ya Kristo inatangaza na kutakiwa kuishi Injili hiyo kikamilifu.

Mantiki nyingine ya Umisionari wa Kanisa, Padre Zagore anathibitisha kuwa: Kanisa ambalo halina huruma, haliwezi kuwa la kimisionari, kwa maana, Kanisa kwa asili yake, ni la kimimisionari na huruma. Huwezi kutengenisha utume wa huruma, kwa maana utume na huruma ni mambo mawili yanayotambulisha Kanisa lenyewe na Utume msingi wa Kanisa ni chombo cha huruma kwa ajili ya ubinadamu!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.