2018-04-09 15:45:00

Pasaka ya Kiorthodox imeadhimishwa tarehe 8 Aprili 2018 !


Wakati Kanisa Katoliki limeadhimisha Pasaka tarehe 1Aprili 2018, baadhi ya nchi kama  Ulaya Mashariki, Ugiriki, Urusi, Romania, Serbia; Burgaria, masedonia Ukraine pia nchi za Masharika wamesheherekea Pasaka ya Kiorthodox tarehe 8 Aprili 2108. Sikukuu hii ilifanyika kwa kina katika jumuiya zote za Kiorthodox Ulaya mashariki na nchi za Mashariki.

Maadhimisho ya Pasaka yamefanyika hivyo kutokana na utofauti wa kalenda ya kijulikani ambapo wakati mwingine inaweza kutofautiana wiki moja au mbili au kufanana, kwa mfano mwaka 2017 sikukuu ya Pasaka katoliki na ile ya Kiorthodox viliadhimishwa pamoja. Sikukuu ya Pasaka kwa Kanisa la Kiorthodox au Kanisa Katoliki kwa kawaida yanafuata maadhimisho yote ya siku Tatu Kuu kabla ya Pasaka kwa kufuata utamaduni wa kitume na kwa maan hiyo,  roho ni ile ile na hata kama karne chache zilizopita, liturujia hizi  zimeendelea kuwa na tofauti.

Katika fursa hiyo ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka, Askofu Mkuu Gennadios wa Kiorthodox nchini Italia na Kisiwa cha Marta pamoja na maeneo ya Ulaya mashariki ametoa ujumbe wake kuwa:Yesu hakufufuka tu katika wafu, bali hata ambaye kashinda mauti. Ni mabadiliko ya wazi kuonesha ufufuko huo ya kwamba ni Mtu aliyeshinda, anafufuka kwa nguvu zaidi imani na matumaini! 

Ujumbe wake unaendeea kusema kuwa,ufufuko wa mwili na mabdiliko ya roho ni vitu viwili msingi wa imani yetu;  hakuna kuzuizi cha kufufuka mwili, lakini kubadilika  kwa roho unahitaji utashi wa binadamu ili kuondokana na dhambi. Kama ulivyo ufufuko wa Mungu na Mwokozi Yesu Kristo unatoa  zawadi duniani utamu na furaha, shangilo la roho na furaha ya kweli ambayo ni ushindi wa maisha dhidi ya mauti na ushindi wa Kristo katika wafu; furaha dhidi ya uchungu, na ukweli dhidi ya ulaghai, kwa maana upendo na umoja vinaungana pamoja!

Katika maadhimisho ya Pasaka ya Kiorthodox, iliyofikia kilele chake tarehe 8 Aprili 2018,  Papa Francisko , mara baada ya Misa ya Jumapili ya pili ya Pasaka, na  ambayo  ilikuwa ni Jumapili ya Huruma ya Mungu;  kabla ya sala ya Malkia wa mbinu, amewatakia matashi mema Kanisa la Kiorthodox ili maadhimisho yao yawe ya furaha na amani kwa wote.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.