2018-04-06 15:52:00

Semina mpya ya SECAM na CCEE kufanyika nchini Ureno: 12-15 Aprili


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE) na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar (SECAM) watafanya semina moja kwa mabara haya mawili inayohusu kauli mbiu ya “matokeo ya utandawazi kwa Kanisa na kwa ajili ya utamaduni Ulaya na Afrika”; semina hiyo itafanyika huko kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Fatima nchini Ureno kuanzia tarehe 12-15 Aprili 2018. Kwa kufuata utashi wa kuhamasisha ukuaji na ushirikiano wa kichungaji katika ya Mabaraza ya  Maaskofu wa mabara haya mawili,ni karibu zaidi ya miaka hivi, vyombo hivi  vimekuwa vikiandaa mikutano na semina mbalimbali ili kuongeza juhudi za umoja, ushirikiano na kuwa na tafakri juu ya changamoto kubwa za Kanisa.

Mada ya utandawazi itawasilishwa na hotuba ya Profesa Livia Franco wa Taasisi ya Mafunzo ya Kisiasa katika Chuo Kikuu Katoliki nchini Ureno. Na baadaye itafuata kazi ya semina itakayogawanyika katika makundi matatu ya kukabiliana na muktadha wa utandawazi katika vijana, wahamiaji, uelewa wa mtu na katika ekolojia ya binadamu.

Kila aina ya mada itakayogusiwa, itakuwa na utangulizi wa hotuba mbili, mmoja akiwa kutoka kwa  Askofu wa ulaya na mwingine kutoka Afrika. Mwisho wa hotuba hizo Askofu wa Ulaya na Afrika watajaribu kuonesha ni jinsi gani wanajikita katika utume wa Askofu mbele ya changamoto za utandawazi. Semina hiyo itahitimishwa kwa kutoa ujumbe wa kazi ya pamoja ya (CCEE na SECAM ).

Semina inafanyika nchini Ureno kwa mwaliko wa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Ureno, Kardinali Manuel Clemente na Patriki wa Lisbon, lakini ambaye pia atakuwa katika semina hiyo kwenye Madhabahu ya Fatima. Askofu António Marto wa Leira  Fatima, atatoa salam za kuwakaribisha katika jimbo mahalia. Na shughuli za mkutano zitaongozwa na Kardinali Angelo Bagnasco Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE), na Askofu mkuu   Gabriel Mbilingi Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar. (SECAM.
Wenyeviti hawa wawili watatoa hotuba yao, tarehe 12 Aprili 2018 katika kipindi cha kwanza cha ufunguzi ambacho kitafanyika huko Lisbon katika Seminari ya  Dos Olivais. 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.