2018-04-03 16:07:00

Wito wa Maaskofu Marekani kwa miaka 50 tangu kifo cha Luther King!


Katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuuwawa kwa baba mtetezi wa haki za raia Martin Luther King, wanajiuliza ni matendo gani ya kuweka katika uwanja wa mapambano hayyo kwa ajili ya utetezi wa ndugu kaka na dada ambao bado wanaendelea kuseka na kubeba uzito wa ubaguzi. Kwa kutafakari juu ya maisha namatendo ambayo Mchungaji Martin Luther King alifanya. Ni lazima kujiuliza, iwapo wanafanya kila liwezekanavyo kwa kuhakikisha ujenzi wa utamaduni wa upendo, heshima na amani ambayo ni kiini cha Injili inavyoelekeza!
 
Maaskofu wa Marekani wameandika ujumbe wao kwa waamini wote na wenye mapenzi mema kwa kutoa tamko kuhusu ubaguzi wa rangi , wakati wa tukio la maadhimisho ya miaka 50 tangu kuwawa LUTHER KING. Na kwa maana hiyo katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuuwawa kwake Baba mtetezi wa haki za raia ni kujiuliza shughuli za kujikita katika kuwatazama ndugu wengi kaka na dada ambao wanazidi kuteseka kutokana na kubeba mzigo wa ubaguzi. Na jinsi gani Mungu anaweza kuwalekeza katika nguvu zao zote kwa ajili ya kusaidia mabadiliko ya moyo hasa kwa wale ambao wanazidi kuongeza chachu dhidi ya mawazo potofu ya ubaguz, aidha katika shughuli ya kujikita kwenye  mapambano dhidi ya ubaguzi?

Ni maswali ya maaskofu hao wa Marekani, wanayouliza mara baada ya matukio mengi ya ubaguzi wa rangi nchini humo ambapo wanakazia juu ya kutafakari suala hili kwa kina.

Siku ya kuuwawa: Martin Luther King aliuwawa tarehe 4 Aprili 1968 huko Memphis, Tenessee. Alifika katika sehemu hiyo kwa ajili ya kutetea waamerika weusi waliokuwa wameajiriwa katika huduma za usafi,lakini wakilipwa mshahara mdogo na kunyanyaswa. Na katika hotuba yake ya mwisho, jioni kabla ya kifo chake, lengo pia lilikuwa ni kulezea juu ya hatari nyingi zilizokuwa zimemzunguka lakini wakati huo na kuhakikisha kuwa yeye angependelea kuishi kwa muda mrefu, lakini la muhimu zaidi ni kufanya kwanza mapenzi ya Bwana.

Mfano wa uvumilivu na  kupinga kutumia nguvu: Maaskofu wa Marekani wanafikiria maisha ya Luther King kama mfano wa kuigwa hasa ule wa uvumilivu na kupinga kutumia nguvu, ambayo ni mambo yaliyo mwongoza daima kuvumilia na mapambano yake mbele ya hatari zilizokuwa zinamzunguka hata madharau au kutojali kutoka kwa watawala nchini humo.

Imani inatufanya tuwe na ujasiri: Maskofu kadhalika wanaandika ya kuwa: imani inatoa msukumo wa kuwa na ujasiri, kujihatarisha wenyewe kwasababu ya kutaka kutetea hadhi ya jirani ambaye ni mfano wa sura ya Mungu. Wanamtaja hata maneno ya Papa Francisko katika ujumbe wao ya kuwa:Papa anakumbusha kuwa “mara nyingi tusikae pembeni mbele ya ubaya ulio mkubwa  au kuzidi kiasi na  hata wakati hatari inayotuzunguka”.

Na ili kumwenzi vizuri Mchungaji Martin Luther King  na katika  kuendeleza urithi wake Maaskofu wanasisitiza kuwa: ni lazima kujikita katika kutafakari kwa kina wajibu wa kufuata mapenzi ya Mungu, mahali popote wanapotumwa, kwasababu Yeye anafanya kazi pamoja na wale wanao hamasisha haki !

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.