2018-04-02 15:00:00

Malkia wa Mbingu:Amefufuka ni tangazo la kwanza kutoka kwa Malaika!


Jumatatu baada ya Pasaka inaitwa Jumatatu ya Malaika kwa mujibu wa utamaduni mzuri sana na ambao unatokana  na chimbuko la kibiblia kuhusu Ufufuko. Injili kwa dhati ya Matayo, Marko na Luka (taz Mt 28,1-10,Mk16,1-7;Lk 24,1-12) wanao wanasema kuwa: wanawake walikwenda Kaburini, wakakuta liko wazi. Walikuwa na hofu ya kuwa watawezaje kuingia katika kaburi ambalo lilikuwa limefunikwa na jiwe kubwa. Badala yake wakakuta kaburi liko wazi; na ndani yake wakasikia sauti isemayo: Yesu hayupo hapo kwasababu amefufuka.

Ni utangulizi wa tafakari  mahubiri  ya Papa Francisko tarehe 2 Aprili 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro, wakati wa sala ya Malkia wa mbingu, tukiwa katika siku ya Pili ya Pasaka. Papa Francisko akiendelea na tafakari hiyo anasema kwamba ni  kwa mara ya kwanza maneno “Amefufuka “yanatamkwa. Injili zote zinasema kuwa siku ya kwanza ya kutoa tangazo, ilikuwa ni kwa njia ya malaika, yaani wajumbe wa Mungu. Na kwa maana hiyo, kuna maana kubwa ya uwepo wa malaika kwani: hata aliyetangaza “Neno kufanyika Mwili alikuwa ni Malaika Gabrieli  na kwa namna hiyo, kutangaza kwa mara ya kwanza Ufufuko, isingetosha tangazo kutoka kinywa cha binadamu. Ilikuwa lazima awepo aliye mkuu zaidi kwa ajili ya kutangaza hali halisi ya namna hii, ya kushangaza na ambayo isingekuwa rahisi kuamini, hata mtu wa kawaida kudiriki kutamka manen kama  hayo! Baada ya tangazo hilo la kwanza, jumuiya ya mitume walianza kurudia wakisema: ni kweli Bwana amefufuka na amemtokea Simoni ( Lk 24,34)na kwa hakika tangazo la kwanza lilikuwa linahitaji akili iliyo ya juu kuliko ya binadamu.

Kile ambacho kinaadhimishwa leo hii, ni kama kawaida yakufanya  sikuuu na  uzoefu wa familia. Baada ya maadhimisho ya Pasaka, kuna haja ya kungana kwa pamoja na ndugu na marafiki ili kusheherekea. Hiyo ni kwasababu udugu ni tunda la Pasaka ya Kristo, ambaye kwa njia ya kifo na ufufuko ameshinda dhambi iliyokuwa inatenganisha binadamu na Mungu, utu binafsi  na kuwa mtu na ndugu zake. Yesu alibomoa kuta za utengenishi kati ya watu na kuimarisha amani, pia kuanza kusuka mtandao wa undugu upya. Ni muhimu sana katika nyakati hizi kugundua undugu na kuuishi kama walivyokuwa wakiishi jumuiya za kwanza za kikristo anasisitiza Papa Francisko. 

Siyo rahisi kuwa na umoja na kujikita kwa ajili ya kutafuta umoja na haki za kijamii bila kuanzia na undugu na mshikamano. Na bila kushirikishana kindugu, siyo rahisi kukamilisha jumuiya ya dhati ya Kanisa au kiraia, kwa maana ni kuongozwa na manufaa na mambo yao binafsi. Na kwa maana hiyo anabainisha tena kwamba, kama ijulikanavyo dhambi daima utengenisha na kutengeneza maadui!

Pasaka ya Kristo imweze kusmbaza  katika dunia, mazungumzo mapya na mahusiano kwa  upya, ambao kwa wakristo wanageuka kuwa wawajibikaji. Kwa dhati Yesu alisema: “pendaneni kama nilivyo wapenda kwa namna hiyo watu wote watawajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu”. Papa Francisko anasisitiza, hatuwezi kujifungia binafsi, katika makundi yetu, kinyume chake, tunaalikwa kujikita katika kutafuta wema wa pamoja na kusaidiana  nandugu, hasa wale wadhaifu na waliobaguliwa. Ni kwa njia ya undugu tu  unaweza kuhakikisha amani ya kudumu na kushinda umaskini, inawezekana kuzima mivutano na vita na inawezekana kung’oa ufisadi na uhalifu.

Malaika aliyeema, “ Amefufuka” atusaidie kuishi undugu na  upya wa mazungumzo, uhusiano na kuangaikia wema wa pamoja. Naye Bikira Maria ambaye kwa kipindi hiki cha Pasaka tunamwomba kwa jina la Malkia wa Mbingu atusimamie kwa sala zake ili undugu na umoja ambao tunafanya uzoefu kwa sikukuu ya Pasaka uweze kugeuka kuwa mtindo wa maisha na kuongoza mahusiano yetu!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.