Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Patriaki Tawadros II amemtumia Papa Francisko Matashi mema ya Pasaka!

Patriaki Tawadros II Mkuu wa Kiorthodox nchini Misri amemtumia Salam za Matashi mema ya Sikukuu ya Pasaka Papa Francisko - ANSA

31/03/2018 12:40

Patriaki  Tawadros II nchini Misri amemtumia salama za Matashi mema ya Pasaka 2018, Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya Video akisisitiza kuwa: “Kristo amefufuka kweli kweli Kafufuka” Ni Sikukuu ambayo wote wanafuraha kwasababu Yesu Kristo amefufuka na ameshinda kifo, baada ya mapambano ya dhidi ya kifo Msalabani na kutoa wokovu maisha ya binadamu wote”. 

Ujumbe huo kwa njia ya Video, umerekodiwa na Shirika la habari Katoliki, Sir katika Makao Makuu ya Kipatriaki mjini Cairo, ambapo Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox na Patriaki wa Alexandria ametaka kutoa matashi mema ya Sikukuu ya Pasaka ili yamfikie Papa Francisko,pamoja na kwamba maadhimisho ya pasaka kwa Waorthodox kwa kawaida wanaadhimisha wiki moja baada ya Pasaka katoliki, na kwa njia hiyo Pasaka yao itakuwa tarehe 8 Aprili 2018, kwa mujibu wa kalenda yao ya Kijuliani.

Katika ujumbe huo anaendelea ksema: “Ninakutakia Sikukuu njema Baba Mtakatifu, ni matarajio yangu kuwa wewe ni mzima wa afya njema na furaha. Ninahitaji daima ya sala zako kwa ajili yetu”; pia  Patriaki Tawadros II ametaka kumtakia salama za matashi mema hata kwa ajili ya kutumiza  mwaka wa tano tangu kuanza utume wake kama kharifa wa mtume Petro ulio hitimishwa hivi karibuni na kusema: “Kwako Baba Mtakatifu Francisko, ninayo furaha ya kutoa ujumbe huu nikiwa hapa nchi ya Misri. Nikukutakia mema na baraka katika mwaka wa tano tangu kuchaguliwa kwako”.

Katika utume wa furaha na uliobarikiwa, siwezi kusahau ziara yangu niliyokuja Roma, miezi miwili baada ya uchaguzi huo mei 2013!  anaendelea Patriaki Tawadros II: “Ilikuwa ni ziara nzuri sana na tulikuwa tumejazwa na Roho Mtakatifu. Ninayo matumaini katika sala zako daima kwa ajili yetu pia hata sisi tunakukumbuka daima katika sala zetu. Bwana aweze kubariki huduma yako, utume wako, afya yako na kukupatia maisha marefu.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

31/03/2018 12:40