2018-03-31 15:01:00

Mapatriaki na Viongozi wa Makanisa Yerusalemu wametoa ujumbe wa Pasaka!


Maombi kuelekeza kwa Mungu kwa ajili ya watu ambao wanatembea katika njia ya msalaba , kwa jili ya wanaoteseka katika kanda yao na dunia nzima, hata watu ambao wanateseka katika ukimya; kwa ajili ya wakimbizi na wanaoomba hifadhi, waliorudikana katika makambi, kwa ajili ya wale wanaoishi kwa kunyanyaswa, wenye kuhitaji na wasio kuwa na hadhi, kwa ajili ya waathirika wa kutumia nguvu, ubaguzi, na kwa ajili ya wote wanaopambania haki na mapatano.

Ndiyo maombi yanayojitkeza katoka katika ujumbe wa Pasaka 2018 ulioandikwa na Mapatriaki na viongozi wakuu wa kikristo huko Yerusalemu, kati yao akiwemp Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki Yerusalemu na Msamamzi wa maeneo ya nchi Takatifu, Padre Francisko Patton, katika ujumbe ulitoangazwa kwa tukio la Pasaka.

Yerusalemu ni mji wa matumaini: “Kutoka Yerusalem mahali ambapo Kristo alifufuka kutoka katika wafu, tunatoa baraza zetu kwa waamini ambao wanaadhimisha sikukuu ya Ufufuko kwa kipindi hiki kilicho barikiwa”, wanaandika katika ujumbe. “Hiki ni kipindi ambacho familia za kikristo katika dunia wanakumbuka kazi ya wokovu wa Mungu katika maisha yaani kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. Yerusalemu, mji wa matumaini na fufuko, na unabaki kuwa ishara ya wokovu wa Mungu na kioo cha Yerusalem mpya ya Mungu ambayo bado na  lazima itatimia.”

Taa kwa ajili ya maisha ya watu: Ujumbe unaendelea kusemeka: “Katika hali halisi, hiyo ndiyo tabia takatifu, ya kijumuiya na tasaufi ya Yerusalemu inayoendela kuwa taa kwa ajili ya matumaini, amni na maisha ya watu wa kanda hiii na dunia nzima. Tuombe ya kwamba sisi tuluiopo Nchi Takatifu tunaweza kuendelea bila vizingiti ili kutimiza wajibu wetu Mtakatifu kama maonesho ya Injili hai kwa ajili ya kutoa  huduma kwa maskini, kutafuta haki na kutembea katuka mwanga na upendo wa Kristo Mfufuka”!

Sr Anglea Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.