2018-03-30 17:08:00

Iraq:Patriaki Raphael Sako awatakia matashi mema ya usalama na msimamo!


Kutoka katika nchi iliyojulikana  ya utukufu na bahati leo hii nchi ya Iraq imegeuka kuwa nchi ya majanga ya ubaya utokanao  na wizi na kuua. Matokeo ya nchi hiyo kwa sasa imepoteza usalama na msimamo wa ustawi wake ikiwemo raia wake kunyenyekezwa. Watu nchini Iraq wanatafuta usalama na msimamo, matarajio ya kiuchumi na utamaanduni. Pamoja na kukumbana na majanga haya hawapaswi kukata tamaa zaidi watazame mbele na macho ya imani. Huo ndiyo ujumbe wa Pasaka wa  Patriaki wa Baghadad nchini Iraq, Louis Raphael Sako alio waandikia waamini wote na wenye mapenzi mema, ujumbe ulitangazwa kwa njia ya mtando wa Kipatriaki.

Mateso ni mkate  wa  binadamu na mtindo wa kukabiliana na hayo yote  utakuwa ni mwelekeo wa utu wao, anathibitisha  Patriaki Sako na kuwaalika washirikiane wote kwa ajili ya maisha endelevu ya nchi na  ili kuweza kushinda utofauti wa dini, kabila , rangi au mantiki za wingi na uchache. Utume wao kama binadamu na waamini ni ule wa kuhudumia wengine kwakuwa wote ni ndugu na sadaka yako kwa ajili yao itazaa matunda. Na kwa namna hiyo anatoa wito wa kila mzalendo kuhisi uwajibikaji kwa kuanzia ule uwajibikaji kimaadili na kitasaufi katika hali hiyo na kuchangia kujikita kwa hali na mali kwa kila aina ya vyanzo binafsi au makundi vinavyojikita katika ujenzi wa amani ya Iraq.

Ili kuweza kushinda matatizo ni lazima kuwa na sababu, kuhamasika katika mantiki ya uzalendo na kuwa na lugha moja ya mazungumzo, upendo urafiki na mshikamano. Aidha  Patriaki Sako kwa maana hiyo,  ujumbe wake pia umelenga juu ya uchaguzi mkuu wa wabunge  utakao fanyika mwezi wa tano, akikumbusha kuwa kupiga kura ni uwajibikaji, kimaadili na kitaifa, hivyo anawaalika wazalendo wa Iraq  wasikose kwenda kupiga kura ili kuweza kutimiza lengo la ndoto zao za kuwa na Taifa moja la  nguvu,  kwa ngazi ya kijamii, kiuchumi , elimu na utamaduni.

Serikali ya raia ambayo inasimamia misingi ya  sheria ya kulinda wadhaifu kwa namna ya kutafuta hata usawa kwa wote. “Iraq kwa upande wetu ni uzalendo wetu na kimbilio letu”. Kwa upande wa dini unatazama Mungu peke yake na ambapo inabidi kulinda hali hiyo bila kuingiza  katika mijadala ya kisiasa” Anasema Sako.

Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.