2018-03-30 15:51:00

Habari iliyotolewa na Gazeti la Repubblica juu ya Papa si ya kuaminika!


Ofisi ya habari  Vatican inatoa maelezo  kuhusu habari uliyotangazwa katika Gazeti la Repubblica nchini Italia  juu ya Papa Francisko alipokutana hivi karibuni na Mkurugenzi wa gazeti hilo kwamba, habari hiyo siyo ya kuaminika kwa mujibu wa  maneno ya Papa kama ilivyotolewa katika Gazeti hilo.

Na kwa mujibu wa Habari kamili Vatican zinathibitisha kuwa, Papa Francisko alikutana hivi karibuni na mwanzilishi wa Gazeti la kila siku la Repubblica  Bwana Scalfari katika  mkutano wa faragha ikiwa ni fursa ya kupeana matashi mema ya  Pasaka, lakini hawakufanya au kuacha aina yoyote ya mahojiano!

Kwa mujibu wa maelezo hayo pia  Ofisi ya habari Vatican, inathibitisha kwamba, kile ambacho kimeandikwa katika gazeti hilo,kifikiriwe kama  ni  tunda la utunzi wa habari binafsi,ambao lakini ahusiki  katika maneno yaliyozungumzwa na  Baba Mtakatifu !

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.