2018-03-28 11:48:00

Salam na matashi mema ya Pasaka kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI


Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu; Jumanne, jioni tarehe, 27 Machi 2018 amemtembelea Papa Mstaafu Benedikto XVI ili kumtakia heri na baraka za Sherehe ya Pasaka kwa Mwaka 2018. Baba Mtakatifu mapema asubuhi, Jumanne tarehe 27 Machi 2018 akiwa ameambatana na Monsinyo Paolo Borgia, ametembelea kwenye ofisi zote za Sekretarieti kuu ya Vatican na kusalimiana na viongozi pamoja na wafanyakazi wao. Baba Mtakatifu alianza ziara ya kutembelea ofisi hizi kwa kubariki ofisi mpya zilizotengwa rasmi, Mwezi Novemba, 2017 kwa ajili ya wafanyakazi katika diplomasia ya Vatican. Baba Mtakatifu amewatakia wote hawa heri na baraka katika maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka kwa Mwaka 2018.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.