2018-03-27 09:02:00

Masikitiko ya Papa kufuatia kifo cha watu kwa janga la moto nchini Urusi!


Tarehe 26 Machi 2018 Baba Mtakatifu ametuma Barua yake  kuonesha maskitiko yake, kufuatia tukio  la moto uliotokea nchini Urusi na kuteketeza kituo cha kibiashara ambapo  watu wengi wamepoteza maisha wakiwemo pamoja na watoto wengi  na wengine kujeruhiwa. Ujumbe wake unawaendea wote walio athirika, ndugu na jamaa waliopatwa na janga hilo katika moto kwa Kituo cha biashara cha Winter Cherry katika mji wa Siberia huko Kamerov nchini Urusi .

Ujumbe wa Papa uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwa niaba yake, anawakabidhi waathirika wote, hasa zaidi watoto ambao wamepoteza maisha kwa upendo wa huruma ya Mungu mwenyezi. Aidha anawakikishia maombi yake wote ambao wanaomboleza kwa ajili ya wapendwa wao na kuonesha  uwepo wake karibu kiroho kwa wote, viongozi wa nchi na wale wote ambao wanaendelea kujikita katika mchakato wa kutafuta wale ambao bado hawajapatikana.


Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.