2018-03-24 14:48:00

Papa anayo shauku ya kutembelea nchi ya Sudan ya Kusini!


“Papa ameelezea juu ya shauku ya kutelemka nchini Sudan ya Kusini ili kuweza kukaa karibu na watu wanaoteseka. Na kwa njia hiyo sisi tunasubiri kujua ni lini wazo hili litatimilika”. Haya ni malezo yalitolewa mjini Roma tarehe 23 Machi 2018 kaika makao makuu ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Mchungaji James Oyet Latansio, Katibu wa Baraza la Makanisa Sudan ya Kusini (Sscc), mara baada ya kukutana na Papa Francisko mjini Vatican.

Mchungaji anaendelea kusema kuwa, kwa hakika wako tayari kumpokea Papa japokuwa hawawezi kusema kuwa wanayo hali ya usalama wa asilimia 100%, lakini iwapo Papa anaweza kuamua kwenda huko kama alivyokwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Myanmar, hata wao wanayo furaha ya kumpokea. Mchungaji Latansio akielezea zaidi katika Shirika la habari  Katoliki  Sir, amegusia hata shauku ya Papa ya kufanya ziara akiwa pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury na viongozi wakuu wa Kanisa la Scotland, kwa maana hiyo utashi wake ni kwamba iwe ziara ya kiekumene.

Wakati wa mkutano na wawakilishi tisa wa Baraza la Makanisa nchini Sudan ya Kusini, Papa amesikiliza kwa makini juu ya hali halisi ya nchi kwasasa, mahali ambapo tangu mwaka 2013 wako na migogoro ya ndani ambayo imesasbaisha watu milioni 7 kuwa na mahitaji ya dharura  na milioni 2 za watu wa Sudan ya kusini kukimbilia katika nchi za karibu (Etiopia, Sudan, Kenya, na Congo DRC).

Aidha wakieleza juu ya muungano kwa ajili ya amani anasema,  wamemsimulia Papa jinsi gani wao wanafanya kazi wakiwa wameungana kwa ajili ya amani. Katika makambi ya wakimbizi wanajaribu kufanya kazi kubwa ili watu waweze kuwa na umoja na mapatano. Na papa amewaeleza jinsi gani anavyo wakumbuka watu wote wa Sudan Kusini wakiteseka, na kwamba, yeye hawezi kuwa na  amani wakati bado kuna sehemu ya Kanisa inayoendelea kuteseka.

Hata hivyo kipindi hiki cha mwisho Baraza la Makanisa Sudan ya Kusini wameanzisha mipango kwa ajili ya kuhamasisha amani kwa msaada wa  njia ya  “Jukwaa la uhai mpya la ngazi ya juu” kutokana  msaada wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Chombo hiki kimetambuliwa na Shirika la Kanda ya Pembe ya Afrika. Baraza la Makanisa Sudan ya Kusini wametoa ushauri kwa washiriki wote ili kuanza kuwashauri viongozi wa Sudan Kusini wasitishe migogoro hiyo. Jumuiya ya Matakatifu Egidio kwasasa inajikita katika mchakato huo wakisaidiana na Baraza la Makanisa Sudan ya Kusini.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.