2018-03-24 14:30:00

Mtandao wa Maji Kiekumene : wasema maji ni haki msingi!


Wakristo wote wanapaswa kuwa upande wa watu maskini na wote wanaobaguliwa ili kuwapatia hata wao uwezekano wa kupata huduma ya  maji salama ya kunywa na kama ishara ya haki katika ulimwengu huu. Ni maneno ya Dineshe Suma, mmoja wa waandaaji wa mpango wa Mtandao wa Maji  Kiekumene unaoratibiwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc), wakati akitafakari juu ya Siku ya Maji Duniani inayoadhimishwa tarehe 22 Machi ya kila mwaka.

Siku ya Maadhimisho ya maji Duniani mwaka huu imeongozwa na mada ya “Uasili wa Maji”, ambayo pia iko katika kalenda ya maadhimisho ya Mtandao wa maji kiekumene na hivyo wakristo ni kama moja ya hatua ya safari ambayo inawaajibisha kila mmoja kulinda kazi ya uuumbaji. Kwa maana hiyo katika fursa hiyo, idadi kubwa ya wito, tamko na maanzisho, ambayo yanahamasishwa kwa roho ya kiekumene, yametendeka ili kuwakumbusha wote na zaidi kuanzia katika jumuiya binafsi, kwamba jambo la kwanza  la maji ni kigezo ambacho ni zawadi ya thamani ya Mungu ambayo amewapatia watu wote, wake kwa waume, zaidi ambao jana na leo wanaendelea kuwa na matatizo ya kupata maji salama ya kunywa na kila  mtu awe na uwezekano wa kupata tunu hiyo msingi.

Kwa upande wa Shirikisho la Kiuteri ulimwanguni linasema kuwa, katika dunia wakristo wanapaswa kutumia muda wao kusaidia wote ili waweze kufikia  hata ngazi ndogo ya upatikanaji wa maji ambayo kwao ni ndoto kutokana na majanga ya asili, kama vile ukame na mafuriko ya kila wakati, zaidi katika umaskini wa ukosefu wa vituo vya afya na wakati huo bila kusahaau hali ya wahamiaji na wakimbizi. Kutokana na suala la wakimbizi, kwa mfano wa kambi ya wakimbizi iliyoko Minawao, Kaskazini ya Camerun, watu wanasimulia hali ya kutisha ya maisha! Hali kadhalikia moja ya sehemu wampenda kukumbuka waluteri pamoja na wakristo wengine, ni  kutafuta njia hasa ya kuendelea kupambana dhidi ya ukosefu wa haki ya maji kwa watu wengi duniani. 

Hata hivyo kwa siku hizi hata Baraza la dunia la Wamenoniti wametoa tamko lao kuhusu hupatikanaji wa maji ya kwamba: ni jukumu la msingi na haki ambazo wakristo wanaweza kuchangia kwa kahamasisha na kupambana dhidi ya kila aina za ubaguzi kwa mujibu wa Injili inavyotaka. Zaidi hata Mashirika ya huduma kimisionari duniani, imerudia kusisitiza juu ya maana ambayo wakristo wanapaswa kuchukua wajibu ili kupambana na kushinda vizingiti vinavyozuia upatikanaji wa maji katika nchi maskini. 

Na katika Jukwaa la dunia kwa ajili ya maji lililoandaliwa na Baraza la Makanisa ulimwenguni(Wcc), ukuu wa washiriki wa Makanisa na Mashirika ya kiekumene, wameonesha kiiini na mwanga wa mipango ambayo imewekwa katika kambi, zaidi kuangaza miaka hii ya mwisho ambapo wanatoa shukrani kubwa kwa mchango na neema ya Waraka wa Papa Francisko waa “Laudato Si” sifa kwa Bwana .

Katika Jukwaa lililofanyika huko Brasilia nchini Brazil kuanzia tarehe 18-23 Machi 2018, Mchungaji wa kiluteri Romi Márcia Bencke, ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni ka upande wa Brazil wakati wa hotuba yake, amewakumbusha nafasi ya Bara la Amerika ya Kusini katika mapambania haki ya maji, kwa kipindi ambacho bara la Amerika ya Kusini linawakilisha asilimia 12% za Maji Duniani.

Anathibitisha akisema, hii ina maana ya kulinda rasilimali, kama haki msingi ya binadamu na ambayo inatakiwa kila mmoja kuipata, kupambania hasa katika mchakato wa kuondoa ubinafsishaji wa maji, ambao unazua hatari ya maji na kuunda migogoro, ubaguzi na kuleta aina mpya za umaskini. Katika Jukwaa la dunia kuhusu maji, wamejadili na kugusia mada nyingi ambazo Makanisa tayari yanatoa mchango mkubwa na makundi ya kiekumene ambayo yana nguvu kutoa sauti kwa niaba ya wale wasio kuwa na sauti, ili kuweza kuongeza ukuu wa kiroho kuhusu maji kama wema wa wote na kwa jina la uaminifu wa Maandiko Matakatifu

Sr Angela Rwezaula 
Vaican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.