2018-03-24 13:57:00

Askofu mkuu Julio Murat ateuliwa Balozi wa Vatican nchini Cameroon


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Julio Murat kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Cameroon. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi. Askofu mkuu Murat alizaliwa tarehe 18 Agosti 1961 huko Karsiyaka, nchini Uturuki. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi akapadrishwa kunako tarehe 25 Mei 1986. Kunako tarehe Mosi, Januari 1994 alianza utume wake wa Kidiplomasia mjini Vatican na amelitumikia Kanisa huko Indonesia, Pakistan, Bielorussia, Autria na mwishoni alikuwa kwenye kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Tarehe 27 Januari 2012, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa kumi na sita, akamteua Monsinyo Julio Murat, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia pamoja na kumpandisha daraja kuwa Askofu mkuu na hatimaye, akawekwa wakfu tarehe 3 machi 2012. Papa Mtsaafu Benedikto XVI akamteuwa tena kuwa Balozi wa Vatican nchini Malawi, hapo tarehe 6 Januari 2012. Sasa ameteuliwa tena na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Cameroon.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.