Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Elimu

Nigeria:Wasichana zaidi ya 100 waliotekwa nyara na Boko Haram wameachwa huru!

Baadhi ya wasichana wa Dapchi nchini Nigeria walioachiwa huru mara baada ya kutekwa nyara tangu 19 Februari na Boko Haramu - REUTERS

22/03/2018 15:51


Unicef imepokea kwa furaha kubwa habari za kuachiwa huru watoto waliotekwa nyara na kikundi cha Boko Haramu tarehe 19 Februari 2018 katika shule ya Dapchi  huko Yobe Kaskazini mashariki ya Nigeria. Watoto hao tayari wako mikononi mwa familia zao na kwa mujibu wa habari,zinazema kuwa, wamerudi watoto zaidi ya 100 wasichana.Mwakilishi wa Unicef nchini Nigeria Bwana Mohamed Malick Fall  anathibitisha kuwa, ni furaha kubwa kuona watoto wamerud katika usalama wa familia zao na  kuondoka katika mikono ya Boko Haramu!.

Bwana Fall hata hivyo anaongeza kusema, Unicef inafanya kazi kwa dhati pamoja na ofisi ya waziri wa vijana katika serikali ya Yobe ili kuweza kuwasaidia wasichana hao na familia zao kwa msaada unaohitajika. Kwa upande wake anasema,katika miezi iliyopita wasichana hao inawezekana wamepata mateso ya kimwili na manyanyaso ya ngono. Wanahitaji msaada mkubwa kwa upande wa familia na jumuiya nzima ili baadaye waweze kuhisi uhakika na kurudi tena shuleni.

Aidha kama Unicef pia inajaribu kufanya kazi na mashirika mengine ya kijamii ili kuhakikisha kila msichana anapokea matibabu binafsi , ikiwa ni madawa na msaada wa kisaikolojia. Aidha wanaonesha masikitiko na uchungu mkubwa kwa wanafamilia ambao watoto wao hawakuweza kurudi nyumbani kwao.
 Pamoja na kusubiri uhakika kamili, lakini taarifa zinaonesha kuwa wasichana watano wamekufa, kwa njia hiyo anasisitiza kuwa, Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa wanashiriki msiba mzito wa familia waliopoteza watoto wao. 

Unicef inarudia kwa upya kutoa wito wao kwa wateka nyara Boko Haram, wawachie wasichana wote waliopotea. Na mwisho Bwana Hall, anabainisha kuwa, mashule yote yanatakiwa kuwa na nafasi za usalama na  kulindwa daima, kwa maana tangu mwanzo wa mwaka 2009, zaidi ya walimu 2,295 wameuwawa, 19,000 ni wakimbizi na karibia mashule 1,400 yameharibiwa!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

22/03/2018 15:51