Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Maaskofu Venezuela:Nchi imegeuka kuwa ngeni hata kwa raia wote!

Nchini Venezuela,watu wanashindwa kujikimu kupata hata mlo wa siku kutokana na hali mbaya ya kijamii,kisiasa na kiuchumi - REUTERS

22/03/2018 15:14

Tarehe 19 Machi ilikuwa ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu na  Baraza la Maskofu wa Benezuela katika fursa hiyo wametuma ujumbe kwa watu wa Mungu na wenye mapenzi mema hasa zaidi, wanawakumbusha viongozi wote wa kisiasa, kijamii na kiuchumi ya kwamba, kile wanacho watendea watu waishi maisha magumu, watambue ya kwamba wanamtendea Yesu mwenyewe.

Katika ujumbe wa maaskofu ambao umefika hata vyombo vya habari katoliki Fides unasisitiza kwamba kwa, nchi ya Venezuela imegeuka kuwa nchi geni kwa kila mzalendo anayeishi ndani ya nchi yake, kwasababu ya kupendelea mfumo wa udikteta, usiotoa haki, usio stahili, wa ufisadi na ambapo sheria iko katika mchezo wa yule anayetaka kubaki madarakani akijinufaisha kutokana na mateso ya watu wasio kuwa na hati.

Nchini Venezuela, hali inazidi kuwa mbaya kutokana ukosefu wa chakula, madawa na bidhaa mbalimbali, zaidi hata ukosefu wa umeme ambao unarudisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya maisha ya kila siku kwa watu, kwa mujibu wa Takwimu ya utafiti ("National Survey juu ya hali halisi ya Venezuela (ENCOVI). Takwimu zinaonesha kuwa, ni familia 9 kati ya 10 hawana rasilimali ya kuweza kununua mahitaji yoyote na hawawezi hata kununua chakula cha siku. 

Kadhalika ujumbe wa Maaskofu wa Venezuela wanakumbusha tena juu ya tamko lao la tarehe 29 Januari 2018 walipokuwa wakishauri Serikali  isikilize kilio cha watu; kwa maana hiyo wanarudia kuomba tena kwamba kilio hicho kisikilizwe! Wanasema, ni masikitiko makubwa  kuona ya kwamba wakati mwingine vinatolewa  vizawadi vidogo ili  kuwafanya watu waendelee kuwa watumwa hadi kufikia kiasi cha kutoweza kuzalisha mali inayowatosheleza kuishi. 

Maskofu wanasisitiza kwamba, hakuna muda wa kupoteza, kwa maana ni muda wa mabadiliko na wanakumbusha kuwa, mwisho wa maisha yetu, mbele ya Mungu wote tutahukumuiwa juu ya upendo tuliyo uishi na jinis tulivyo tenda wajibu wetu. Wanawaonya viongozi walioko madarakani wajishushe chini na kuwatazama watu wao maana madaraka hayo yana kikomo na maana wanaweza kupoteza wakati wowote!

Maaskofu mchini Venezuela, wanahimiza kuonesha matendo ya dhati na yanye maana, hasa huruma na upendo kwa wale ambao kweli wanahitaji upendo, huruma na mshikamano, na  kwa namna ya pekee katika wiki kuu  kabla ya Pasaka, ili waweze kuwakumbuka wote ambao wameuwawa wakitetea demokrasia ya nchi yao. Ni matarajio yao kwamba, mwanga na hekima ya Roho Mtakatifu inaweza kuwasindikiza ili kuondokana na kipeo hicho cha kibinadamu katika nchi yote ya Venezuela kwa hali ya haki, amani.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

22/03/2018 15:14