Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Askofu Mkuu Jurkovic:Heshima ya kila mtu na haki zake lazima zilindwe!

Askofu Mkuu Jurkovic anasema Mpango wa Kazi kwa jitihada pana za Umoja wa Mataifa pia ni kukomesha ubaguzi wa rangi, imani au dini na kulinda haki za binadamu. - RV

22/03/2018 15:01

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican  katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine mjini Geneva ametoa hotuba yake tarehe 21 Machi 2018 ambayo inahusu Programu ya Utendaji, na ili kuweka  utaratibu wa kufikia hatua ya kubeba mzigo kwa usawa zaidi na kugawana majukumu ya wakimbizi. 

Askofu akikumbuka maneno ya Papa Francisko, anathibitisha kuwa, Vatican inayo matumaini ya kwamba, juhudi hizi, zitatoa  matokeo mazurui  yanayotakiwa na jumuiya za ulimwengu zinazoongezeka zaidi kwa kuzingatia kanuni za ushirikiano na msaada. Katika hali halisi ya sasa kimataifa, njia na maana  ya njia hazipo za kuhakikisha kwamba kila mtu na kila mwanamke duniani anaweza kufurahia mazingira ya maisha yanayotakiwa na mwanadamu. Kukaribisha na kulinda wakimbizi ndiyo lakini majukumu ya kawaida ya jumuiya yote  ya kimataifa. 

Aidha anasema wakati wa kuitikia mahitaji yao, inafahamika vizuri kwamba umoja huu haufanyo bila sadaka. Katika matukio, wakimbizi hata idadi kubwa ya wakazi wa meneo mahalia wanahusika  katika changamoto hizi zilizo wazi. Nchi zinazopokea na kukaribisha wakimbizi, mara kwa mara na kwa muda mrefu, hutoa mchango mkubwa kwa manufaa ya pamoja na kwa sababu ya ubinadamu, na hufanya hivyo kutokana na rasilimali zao ndogo. 

Kwa njia huyo uwakilishi wake pia ni  kutambua na kupendekeza ya  kwamba asimu inayopendekezwa ya usambazaji wa rasilimali za kifedha kwa maendeleo katika sehemu za taasisi za kimataifa, na kuzingatia umaalum wa miradi, katika nchi zinazowakaribisha wakimbizi, ziweze kuwanufaisha na wakimbizi na kutoa mshikamano kwa  wema na ukarimu wa familia na jumuiya mahalia. Baada ya kufanya hayo yote ndiyo inawezakana kuwekeza katika ubinadamu na amani, kwa ajili ya manufaa ya wote.

Askofu hata hivyo anakumbuka maneno ya Papa Francisko kuhusu wakimbizi ya kuwa: “inabidi kuzingatia akilini ya kwamba wakimbizi si namba za kugawanywa na zilizotengwa, bali ni watu wenye jina, historia  na matumaini ambayo ni matarajio ya maendeleo ya binadamu, lakini ambao wamelazimika kukimbia nchi yao na wanahitaji ulinzi na msaada”. Usambazaji wa fedha na rasilimali haipaswi kutumiwa kama kisingizio cha kutenganisha jukumu la ulinzi kwa nchi fulani tu kwa sababu ya ukaribu wao wa kijiografia na maeneo yasio na uhakika. Wala haipaswi kuwa sahihi kwa vikwazo vya mwendo wa wakimbizi, lakini kiukweli kuonyesha ushirikiano wa kweli wa kimataifa kwa lengo la wazi. (Hotuba ya Papa Francisko kwa wanadiplomasia tarehe 8 Januari 2018). 

Hatimaye Askofu Mkuu Ivan anasema ujumbe wake unakubali kipengele cha aya ya 12 ambacho kinaunganisha Mpango wa Kazi kwa jitihada pana za Umoja wa Mataifa ili kukomesha ubaguzi, kwa mujibu wa rangi, imani au dini ili kuhamasisha na kulinda haki za binadamu.
Kwa dhati anaongeza, ni muhimu kwamba “Compact Global” iwe imara kuhusu mtu, ili kuweza kuepuka mambo yoyote ya kiitikadi, ikiwa ni pamoja na wale wanaojihusisha na umri, jinsia na utofauti. Katika suala hili la mwisho wanapenda kupendekeza  kuwa, heshima ya kila mtu na haki zake za msingi za kibinadamu zinapaswa kuongoza na kuimarisha katika nyanja zote za Mpango wa Kazi.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

22/03/2018 15:01