Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Elimu

Siku ya Maji Duniani:Kila dakika mtoto anakufa kutokana na suala la maji!

Shirika la Saidia Watoto, linatoa ripoti kuwa kila dakika moja, mtoto anakufa kutokana na suala la maji - ANSA

21/03/2018 15:19

Katika kuadhimisho Siku ya Maji duniani kwa mwaka 2018, Shirika la Saidia watoto ( Save the  Children) wametoa ripoti ya kuwa, kila dakika moja mtoto mmoja anakufa kutokana na suala linalohusu maji na ukosefu wa huduma ya bora ya afya unachangia  kifo cha mtoto mmoja kati ya 5.  Asilimia 8% ya watoto chini ya umri wa miaka 5 wanapoteza maisha kwasababu ya magojwa ya kuhara yatokanayo na maji. Vilevile vyanzo vya vifo vya watoto ni kuhusiana na magonjwa mengi yatokanayo na maji, yaani kutokana na ukosefu wa rasilimali yenye thamani kubwa hiyo na vituo vya kutoa huduma ya afya. Shirika la Saidia watoto, (Save the Children) limetoa ripoti hiyo arehe 21 Machi, siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani kwa Mwaka 2018, itakayofanyika tarehe 22 Machi 2018 inayo ongozwa na kauli mbiu “Uasili wa Maji”!

Lengo kuu la mwaka huu ni kuhamasisha na kutoa mapendekezo ya kutafuta suluhisho la uasili ili kuepuka mafuriko, ukame na uchafuzi wa maji. Na katika ripoti kwa ngazi ya dunia inaonesha kuwa, mtu mmoja kati ya watatu hawezi kupata maji salama na mtu mmoja kati ya tisa, hawezi kupata huduma nzuri ya Afya, kwa maana maji hayo yameambukizwa kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Saidia Watoto, (Save the Children) ambalo tangu mwaka 1919 limekuwa na mapambano ya kutaka kuwasaidia watoto ili kuhakikisha maisha yao endelevu. Moja na magonjwa ya kuambukizwa ni yale ya kipindupindu, kuhara damu, taifodi, pum una kuharisha, ambapo suala la kuharisha limekuwa sugu kwa watoto hasa kila siku wanakufa watoto karibu elfu moja chini ya miaka 5 na kwa mwaka mzima ni watoto 361.000.

Mkurugenzi mkuu msaidizi wa Save the Childrenm, Bi, Daniela Fatarella anasema, tayari milioni 159 ya watu wanachota maji katika maziwa, mabwawa, na mito wakati huo kufikia mwaka 2025 nusu ya watu hao duniani wataishi mahali ambapo hakuna maji. Ni lazima kufanya juhudi chini juu ili kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watu hao wanaweza kupata rasilimali hiyo msingi na hali ya usalama katika huduma ya usafi. Haiwezkani kukubali kila mwaka mamia elfu ya watoto wakafa kwa magojwa yatokanayo maji.

Kutokana na suala la moja kwa moja juu ya maji yaliyoambukiza, inahesabiwa kuwa mamilioni ya watu wanachota maji katika vyavyo vya maji machafu, kuongeza suala la ukosefu wa usafi na maeneo ambayo watu hawana maji ya kutosha wakati huo huo, hakuna juhuidu hata za kuweka kipaumbele. Na mbele ya ukosefu wa maji hawafikiri kwa mfano hata kufanya ishara ndogo ya kuwawa mikono, ambapo imesababisha zaidi katika magonjwa ya kuhara watoto kufikia asilimia 53%, na pumu ugonjwa wa pumu asilimia 50%.

Katika bara la Afrika hasa ya Mashariki, kwa namna ya pekee ukame na janga la kuharisha, limesababisha hali kuwa mbaya kwa mwaka mwaka 2017 kati ya miaka yote ya mwisho. Ukosefu wa kulima na vifo vya wanyama kutokana na ukoefu wa maji imesababisha ukosefu wa chakula kwa watu milioni 21 nchini Somalia ikiwemo milioni 1,2 ya watoto kupata utapia mlo. Nchini Ethiopia ni milioni tatu ya watoto, wajawazito au wanaonyonyesha kukosa chakula na kati ya watoto 333.500 kuwa na utapia mlo. Nchini Kenya karibu watoto 483.000 na Sudan ya Kusini milioni moja ya watoto na wajawazito.

Akihitimisha Mkurugenzi msaidizi wa Save the Children Bi Daniela Fatarella anasema, matokeo ya ukame kwa upande wa watoto ni kubwa mno ambayo inahatarisha hata vituo vya afya. Nchi zilizo kumbwa kwa uzito zaidi kwa matukio hayo kama vile Somalia mahali ambapo tayari wako chini ya majanga na manyanyaso. Kuna dharura kwa namna ya pekee kusaidia familia ambazo wakati mwingine wametengana, kunyanyaswa kwa watoto na ukosefu wa elimu!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

21/03/2018 15:19