2018-03-20 15:38:00

Askofu Mkuu Paglia, mwilisheni furaha ya upendo katika familia!


Kanisa halina mpango wa kushutumu familia adharani wala kuwa mahakama ya kuhukumu udhaifu wa maisha na wito wake. Haya yamethibitishwa na Askofu Mkuu Vincenzo Paglia Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya maisha na Kansela wa Taasisi ya Kipapa  Yohane Paulo II, Taasisi  ya Taalimungu  na Sayansi ya ndoa na Familia yenye kuwa na matawi mengi, kati ya matawi hayo hata kituo cha huko Querétaro nchini Mexico.  Katika ziara yake amesindikizwa na Monsinyo Pierangelo Sequeri, Mkuu wa Taasisi ya Yohane Paulo II ambaye tangu 15 Agosti 2016 aliteuliwa na Papa Francisko.  Askofu Mkuu Paglia akiwa katika kituo cha   Querétaro cha utafiti wa kijamii (Cisav) ametoa hotuba yake ya kwanza juu ya matibabu mbadala na semina kuhusu Waraka wa Amoris Laetitia yaani “Furaha ya upendo ndani ya Familia”.

Akitoa ufafanuzi wa waraka wa Papa Francisko kuhusu Amoris Laetitia anasema, ni lazima kuusoma na kuuelewa kwa kina ili kuweza kushinda vikwazo na migogoro kati ya mafundisho na matendo ya kichungaji. Akifafanua zaidi anathibitisha kuwa, Kanisa halijihusishi na shughuli ya kushutumu na kuhukumu mafarakano ya mahusiano au kuwa wawakili wa kuorodhesha matendo makamilifu na yasiyo timilifu.Badala yake, Kanisa linajikita zaidi kutazama mitindo mipya ya kichungaji ambayo inaanzia na mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke na katika sekta zote kuhusu familia, kazi, maisha ya kijamii na uchaguzi binafsi kwa nia ya kuwasaidia kukua kiroho katika maisha yao. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia anasema, ni lazima kujikita katika mantiki ya huruma ya Mungu kichungaji ambayo ndiyo mwongozo mkuu wa waraka wote wa Amoris Laetitia. Kwa njia hiyo, utambuzi wa kina ni muhimu hasa ule wa nguvu ya kichungaji ili kuwaimarisha wanandoa zaidi badala ya kuona udhaifu wa kichungaji.

Akitoa semina siku ya pili juu ya mada ya  matibabu mbadala, Askofu Mkuu Paglia ameweza kuwakilisha hasa mapendekezo 13 yaliyotolewa  wakati wa mwisho wa Mkutanowa Baraza la Kipapa la Maisha uliofanyika hivi karibuni mjini Vatican ambao ulikuwa unachangia hoja ya jinsi gani inapaswa dhamiri maalumu ya madaktari, wanasayans, wauguzi, watu wa kujitolea, wanasiasa, watafiti na ili waweze kujikita kweli katika utamaduni wa kweli wa matibabu mbadala. Kadhalika kumsaidia mtu mgonjwa na kumsindikiza wakati  wa siku za mwisho wa maisha yake; kushinda tofauti zilizopo kati ya Kaskazini na Kusini mwa dunia, ambapo walitafuta kutafakari ni kwa njia zipi wote wanaweza  kupata matibabu, na zaidi pia juu ya  ukosefu wa mafunzo hasa katika mafunzo ya sekta nyeti kama hiyo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.