2018-03-19 16:19:00

Utangulizi wa Kitabu cha Pérez na Scaraffia kuhusu Papa Francisko wa Marekani!


Waandishi wawili Silvina Pérez na Lucetta Scaraffia wamendika kitabu cha "Papa Francisko, Papa  wa Marekani”. Ni kitabu kinacho jihusisha zaidi katika  maisha na mawazo yake, hasa mtazamo wa fursa ya tukio la  miaka mitano ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake kuwa Papa, pia  juu ya maandishi yake mwenyewe mwaka 1990, yanayo husu historia ya wito wake. Kitabu hicho kitawasilishwa tarehe 26 Machi 2018 katika Chuo Kikuu Katoliki cha Sacro Cuore Milano Italia. Atakaye toa utangulizi ni Gombera wa Chuo hicho Franco Anelli na kati ya wengine watakaotoa hoja ni pamoja na Kardinali Gualtiero Bassetti Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Italia.

Gazeti la Osservatore Romano, limetoa utangulizi kidogo kuhusu Kitabu hicho na kwamba,  tarehe 9 Machi wakati wa Mkutan  kwa Wakuu wa Mashirika, Papa Franciskp alikuwa amezungumza  nao kwa dakika chache, lakini maneno yake yalitoa utamu wa furaha ya uinjilishaji uliokuwa umetolewa na Mwenye heri Paulo VI ambaye baadaye Papa kwa miezi michache aliongozwa na kutoa  Waraka wa “Evangelii Gaudium” (Furaha ya Injili). Huo ni waraka mrefu ambao ni kama mwongozo wa shughuli za kichungaji za Papa Francisko.

Kanisa linaalikwa kwenda nje (pembezoni),kwenda maeneo ya pembezoni, haina maana ya maeneo ya mbali kijiografia, bali ni kuanzia katika maisha ya dhati ya binadamu, ni kutazama fumbo la dhambi, uchungu, ukosefu wa haki, ujinga na ukosefu wa imani, aidha kujilinda dhidi ya mawazo potofu na kila aina ya udhaifu wa maisha ya kibinadamu. Pia katika sura za mwisho za kitabu hicho, zinaonesha wazi mwelekeo wa shughuli  za kichungaji, hivyo ni kutaka kuonesha ya kwamba ni mtu anayejikita kutafakari Yesu Kristo, kuadubu Yesu Kristo, kusaidia Kanisa liweze kutoka ndani yake kuelekea katika maisha  halisi ya binadamu .

Ni papa wa kimisionari kama ilivyojionesha katika maneno yake ya kwanza ambayo yalifanana na yake ya Mtakatifu Yohane Paulo II. Kwa maana yeye alisema ni “Askofu wa Roma kutoka nchi ya mbali” na Papa Francisko mara baada ya kuchaguliwa kwake alisema, ni  “ Askofu wa Roma aliyechukuliwa kutoka karibu mwisho wa dunia”. Ni muhimu kuona kuwa Papa Francisko ni mmisionari kwa dhati kutokana na maisha yake, na ambaye alielimishwa katika tasaufi ya Kijesuit kipindi cha Mtaguso wa II wa Vatican, japokuwa ni Papa wa kwanza ambaye hakushiriki Mtaguso II wa Vatica lakini aliyeonja na kushibishwa na Mtaguso huo kwa maana hiyo ni mtoto kamili wa mtaguso huo.

Kitabu kifafanua juu ya maisha yake: anatambuliwa kuwa Papa Francisko ni mzaliwa wa Argentina katika familia ya wahamiaji kutoka Italia ya Kaskazini, na kubatizwa, tarehe 25 Desemba 1936, siku nane baada ya kuzaliwa, na kwa maana hiyo unaweza kufikiria ni daraja kati ya dunia ya zamani na mpya au kusema mwisho wa dunia kwa mujibu wa maneno yake ya kwaza katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Papa Francisko alijiunga katika shirika la wajesuit tarehe 21 Septemba 1954 kabla ya kutambua njia yake ya maisha ya kiroho ambayo yameweza kumfikisha leo hii mahali alipo. Papa Francisko anajieleza hata katika historia yake ya wito, ambayo yeye mwenyewe aliandika katika barua yake ndefu 1990 kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu. Alichagauliwa kuwa Askofu msaidizi wa Buones Aires 1992. Na mwanzo wa mwaka 2001 kuwa Kardinali.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.