2018-03-17 10:25:00

Ziara ya Papa Francisko Pietrelcina: Igeni mifano ya Padre Pio!


Ninafurahi kutembelea sehemu hii mahali ambapo Francesco Fogione, alizaliwa na kuanza maisha yake marefu, yenye kuwa na  matunda katika  maisha ya kiroho. Katika jumuia hii alitafakari kwa dhati ubinadamu,akajifunza kusali na kutambua maskini katika mwili wa Bwana. Ili ufuasi wa Kristo uweze kukua kwa dhati   aliomba kuingia katika shirika la mafrateli Machapuchini na ndipo akawa Pio wa Pietrelcina. Huo ni utangulizi wa hotuba ya Papa Francisko mara baada ya kufika Pietrelcina, asubuhi ya tarehe 17 Machi 2018, akiwa katika ziara ya kitume katika ardhi alizaliwa Padre Pio, Padre anayejulikana katika ulimwengu kwa matendo yake ya unyenyekevu na kwa njia ya maombezi yake.

Akiendelea na hotuba yake Papa Francisko anasema, Padre Pio alikuwa analipenda Kanisa na matatizo yake, na vikwazo vyake na dhambi zetu zote, kwa maana wote tu wadhambi na tuna aibu, lakini Roho wa Mungu alimwita katika Kanisa hilo  huyo Mtakatifu. Yeye alipenda Kanisa lake Takatifu na wana wake wote wenye dhambi. Akikumbuka kwa upendo mkuu wa Mtakatifu Padre Pio, ambaye ni mfuasi wa Mtakatifu Francisko wa Azizi, amewasalimia wazalendo wote, maparoko, madiwani, mameya wa mji , pamoja na Askofu Felice Accrocaca wa Jimbo hilo na jumuiya nzima ya Wakapucini ikiwa ni pamoja na waamini wote walifika mahali pale.

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amesema kuwa, yeye binafsi anajikuta ameunganika  pamoja nao katika ardhi ya Padre Pio ambaye alikuwapo tangu Septemba 1911 ili kuweza kuvuta hewa nzuri. Enzi zile hapaukuwa na madawa ya kukinga na kuzuia magonjwa na hivyo  magonjwa yalikuwa yakitibiwa katika nyumba ya mama yaani kurudi kujijini  ili kula mambo ambayo ni mazuri, kuvuta hewa ya nyumbani na kusali. Na ndiyo ilikuwa tabia ya kila mzalendo wan a hata yeye ambaye kamwe hakuweza kuacha uasili wake na hata familia yake.

Amepitia kutazama juu ya maisha yake kwamba afya yake hakikuwa nzuri kipindi hicho na mara nyingi alisumbuliwa sana katika nafsi yake akifikiri kutumbuka katika dhambi, kwa maana mara nyingi alipatwa hisi za kushambuliwa na shetani. Alikuwa na mapambao makali na shetani na hivyo hsia nyingi hazikumpatia Amani.Lakini mara moja alipokuwa akisali kwa nguvu na Yesu , hisia hizo zilitoweka. Ameuliza kama wao wanaamini uwepo wa shetani. (wtu walijibu kwa wasiwasi na ndiyo akasema kuwa:atamwambia Askofu awafanyie katekesi. Amerudia tena: je yupo au hayupo shetani? ( waamni wamejibu ndiyo). Baba Mtakatifu amesema, ndiyo shetani yupo, yeye anakwenda pembeni najiingizandani mwetu,na kutudanganya. Kwa njia hiyo Padre Pio alikuwa anaogopa shetani asije mkabili na kumwangusha katika dhambi.Vilevile Papa amesisitiza juu ya hisotria ya Padre Pio wakati anasali alikuwa mara nyingi anashambuliwa na mawazo mabaya ya shetani, lakini mara aliweza kushinda iwapi alijikita kumtazama Yesu kwa ndani mawazo hayo yalipotea.

Na ndipo amefafanua kuwa, hapo kuna taamimungu. Maana hisia zilikuwa “wewe una matatizao, wewe ni mwenye huzuni, wewe ni mgonjwa”. Lakini yote hayo Padre Pio aliweza kuyakabidhi katika mikono ya Yesu na ndiyo shughuli ambayo aliifanya na kuwa na matumaini pekee kwa Yesu.
Ndugu Frateli mnyenyekevu huyo, Papa anafafanua zaidi kuwa  alishangaza ulimwengu mzima katika maisha yake yote kwa maana alijikita katika sala, kusikiliza ndugu kwa uvumilivu mahali ambapo alishiriki mateso yao kama dawa ya upendo kwa Kristo.

Kwa kuiga mifano ya shujaa huyo na fadhala zake, anaongeza, wote wanaweza kuwa vyombo vya upendo wa Mungu , upendo wa Yesu kwa wadhaifu. Na wakati huohuo kwa kufikiria uaminifu wake kwa Kanisa, wote wanaweza kutoa ushuhuda wa umoja, kwasbabu ni umoja tu ambao unaweza kuwafanya wote waishi katika muungano kati yao; ni muungano tu ambao unaweza kudumishwa na kujenga. Maeneo ambayo watu wanapiogana kila siku kamwe, siyo rahisi kujenga, bali watu kuogopa na ni maeneo ambayo yameugua. Amani kati yao na umoja kati yao unahitajika, lakini pia kuwa makini na kujilianda na masengenyo, kwa maana anasema yule anayehisi kusengenya mwingine ni bora ajiume ulimi wake, hiyo itawasaidia kuishi vema ndani ya mioyo yao, japokuwa ulimi utakuwa umevimba lakini ni kwa ajili ya wema wao na kwa  maeneno yao.

Hata hivyo Papa Francisko vile vile amewatakia matashi mema ya kuchota mafundisho kutoka kwa Padre Pio, hasa katika kipindi kigumu cha sasa, kutokana na watu wengi kuwa wazee, vijana kulazimika kuhama ili kutafuata kazi. Papa amehimiza watazame Mtakatifu ili aweze kuwapa mwelekeo wa dhati kwa ajili ya wakati endelevu, kwa  matumanini ya kizazi kipya na umakini wa huruma kwa wazee, ambao ni uruthi wa jumuiya. 

Wazee, Papa anathibitisha ni tunu msingi na  hekima. Akigusia juu ya hekima,ameongeza kusema: Yeye binasi anapendelea kusikia kuwa mara moja wametoa Tuzo ya Nobel ya wazee wakati wa kuadhimisha  siku ya kumbukumbu ya ubinadamu. Mwisho Papa amehimiza jambo msingi la kutunza ushuhuda wa kinabii  wa kikristo na ukuhani wa Padre Pio wa Pietrelcina ; na ili kwake yeye awe chachu kwa wote ya kuishi kikamilifu katika maisha yao kwa mtindo wa heri  katika  matendo ya huruma!

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.