2018-03-17 15:04:00

Sala,udogo,hekima ni kitovu cha mahubiri ya Papa huko San Giovanni Rotondo!


“Katika masomo ya Biblia yaliyosomwa, ninataka kujikita katika maneno matatu: sala, udogo na hekima”.  Ni utangulizi wa mahubiri ya Papa Fancisko wakati wa kuanza mahubiri yake wakati wa Misa Takatifu katika uwanja mkubwa Kanisa jipya la Mapadre Pio wakati wa ziara yake San Giovanni Rotondo, tarehe 17 machi 2018. Papa Francisko akianza kufafanua juu neno la kwanza kuhusu sala anasema: Injili ya siku inaonesha Yesu anasali. Maneno kutoka moyoni mwake “ninakushuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi” ( Mt 11,25). 

Maombi ya Yesu yalikuwa yanamtoka bila  kujiandaa, hakuwa na uchaguzi wowote zaidi ya huo na ndiyo maana wakati mwingine anaonekana  akienda pembezoni akisali hata huko jangwani( Mk 1,35). Mazungumzo na Baba yake ndiyo yalikuwa mstari wa mbele. Na ndiyo maana mitume wake waligundua asili hiyo na kumwomba  awafundishe kusali ((Lk 11,1). Papa Francisko anasistiza kwamba, iwapo tunataka kumfuasa Yesu tuanzie hata sisi mahali Yeye alipoanzia yaani katika sala.

Tunaweza kujiuliza kama wakristo je tunasali  vya kutosha? Mara nyingi Papa anasema, tunapokuwa tunasali, ndipo vishawishi vyingi vya samahani vinajitokeza.na dipo dharura zinajitokeza!  Wakati mwingine ni kuweka pembeni sala kwasababu ya shughuli nyingi zisizoisha na kusahau sehemu iliyo bora (Lk 10,42), shughuli hizo zinakusahulisha kuwa, bila yeye huwezi kufanya kitu (taz Yh 15,5). Miaka 50 tangu Padre Pio anarudi mbingu, Papa anaongeza, anatukumbusha umuhimu wa kuwa na urithi wa sala alio tuachia. Yeye mwenyewe alikuwa akiwasihi watoto wake wa kiroho wasali sana yaani kusali bila kuchoka.( Mkutano wa kimataifa wa makundi ya sala tarehe 5 Mei 1966).

Yesu mwenyewe anaonesha jinsi gani ya kusali: hawali ya yote anaanza na sifa: “ninakushukuu Bwana” lakini kwanza hasemi nina shida ya hiki na kile, Yeye anasema “ninakushukuru”. Hiyo ni kuthibitisha kuwa, siyo rahisi kutambua Baba wa mbinguni bila kujifungua moyo wa shukrani, bila kutumia muda wako kukaa naye na bila kuabudu. Hayo ni mawasiliano binafsi kwa kukaa mbele ya Bwana kusali kwa kimya, Yeye ambaye anaona sirini, ambaye anaweza kuingia ndani mwa roho yako na kufanya muungano pamoja naye.

Ndiyo sala inaweza kufanyika na kuomba msaada, lakini kwa utambuzi kwanza wa kutoa shukrani na kuabudu. Kwa njia hiyo inawezekana kabisa kufanya sala binafsi kama Yesu anayezungumza kwa uhuru wake na kusema, “Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako” (Mt 11,26). Ndiyo mazungunzo huru na  matumaini, sala ya uzoefu wa maisha yote ukiwa mbele kwa Mungu.

Papa Francisko amehimiza kujitazama hasa wakati wa kusali ,iwapo tunasali tunafanana na Yesu, au tunasali wakati tukiwa na dharura? Padre Pio alitambua kusali na kubisha hodi katika moyo wa Yesu ambao inafungua mlango wa huruma kwa binadamu, kwa maana Pade Pio aliacha makundi ya maombi ya sala na kuendeleza kuwa sala ya  nguvu ambayo inaleta  umoja kwa wote wenye mapenzi mema, sala ya kutingisha ulimwengu na kupyaisha dhamiri, sala inayotibu wagonjwa, inayotakatifuza kazi, inayowatuliza wenye nguvu, wanye amani na kutoa nguvu za maadili, sala inayosambaza tabasanu na baraka za Mungu wa kila mnyonge na mdhaifu. Ni vema kutunza maneno hayo na kujiuliza jinsi gani wanasali, wanasifu, wanaabudu na kupeleka maisha mbele kwa Mungu.

Papa akifafanua neno la Pili juu ya “udogo”, anatazama Injili Yesu anayesifu Mungu kwasababu ya kuwaonesha fumbo la  ufalme wa Mungu walio wadogo. Je wadogo ni wakina nani wanaopokea siri za Mungu? Wadogo ni wale wenye kuhitaji wakubwa, ni wale wasio jitosheleza na ambao hawafikirii kujitosheleza wenyewe. Wadogo ni wale wenye moyo wa unyenyekevu, wako wazi, ni maskini na wahitaji ambao wanahitaji ulazima wa kusali na kujiachia wasindikizwe. Moyo wa wadogo hawa ni kama ule wa antena za kunasa mawimbi ya  mawasiliano ili kuweza kunasa sauti ya Mungu. Mungu anatafuta kuwasiliana na wote lakini si kwa wale ambao wanajifanya kuwa wakubwa maana mawimbi yao ya mawasiliani yanachafua mawimbi mengine, maana hao wanajisikia na hawana nafasi ya Mungu. Na ndiyo Maana yeye anapendelea walio wadogo na kuwaonesha njia ya kukutana naye hasa ile ya kuinama na kuwa mdogo kwao, kujifanya mwenye mahitaji. Fumbo la Yesu tunaloliona katika Ostia ya kila misa ni maajabu ya udogo, ya upendo mnyenyekevu, inayoweza kutambuliwa tu kwa kujifanya mdogo na kuwasaidia wali wadogo. 

Kwa njia hiyo Papa anahimiza kujiuliza kama kweli tunatambua kutamfuta Yesu mahali anapo patikana. Kwa maana anasema sehemu ile  kuna dhabahu maalumu ili kuweza kuwatembelea walio wadogo ambao ni wapendwa wa Bwana. Mtakatifu Pio aliita sehemu hiyo kuwa ni “ hekalu la sala na sayansi”, mahali mbapo wote wanaliikwa kuwa watunzaji wa upendo kwa wengine  (Hotuba ya uzinduzi wa nyumba ya wagonjwa  tarehe 5 Mei 1957). Kwa wagonjwa ndipo kuna utunzaji wa upendo kwa yule anayeinama katika majeraha ya jirani, ipo njia ya kukutana.  Anayejikita kuwasaidia wadogo ni sehemu ya Mungu na kushinda utamaduni wa ubaguzi, ambao ni kinyume. Anashinda watawala wasio jali maskini. Na anayependelea wadogo anatangaza unabii wa maisha  pia  manabii wa kifo kwa kila nyakati.

Halikadhalika Papa anasema, hata leo hii wanabagua watu, watoto na wazee kwasababu wanasema, hawasaidii au kuzalisha kitu. Ametoa mfano mmoja binafsi: Tangu utoto wake walikuwa wanafundishwa shuleni historia juu ya ubaguzi. Na kwamba alishangazwa na mwalimu akisimulia kuwa alipokuwa anazaliwa mtoto wa kiume au kike mlemavu walikuwa wakumtupa ili wasiwepo wadogo kama hao. Kwa nji ahiyo wakiwa watoto walikuwa wamasema, jinsi gani watu hao walikuwa ni wakatili.  Papa ameongeza kuwa,lakini hata  leo hii ukatili huo unafanyika  na sayansi. Hilo halihitajiki kwa sababu ya kutozalisha. Huo ndiyo utamaduni wa ubaguzi, wadogo kama hao leo hii Papa anathibitisha hawapendwi na ndiyo maana Yesu anawapendelea hao.

Mwisho Papa Francisko amefafanua juu ya neno hekima. Katika somo la kwanza Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; kwa maana hiyo hekima ya kweli haikai kwa wale wenye uwezo,na nguvu. Ukweli haukai katika nguvu. Hana hekima anayejionesha kuwa na nguvu, aidha hana nguvu anayejibu ubaya kwa ubaya.

 Silaha ya hekima ni upendo ambao unaoongozwa na imani  kwasababu imani ina uwezo wa kuondoa nguvu za ubaya. Padre Pio alipambana na ubaya katika maisha yake yote na alipambana kwa  hekima kama Bwana, kwa unyenyekevu na utii, kwa msalaba akitikia mateso yake kwa upendo. Ni wengi wanashangazwa na hayo, lakini ni wachache wa kufanya hivyo. Akifafanua hilo anasema, wengi wanaongea vizuri lakini ni wangapi wanaiga? wangi wako radhi kuweka anapenda katika picha za watakatifu wakubwa, lakini ni nani anaiga mifano kama wao? Hiyo ni kutokana na kwamba maisha ya kikristo siyo kusema nina penda bali ni ninajitoa zawadi. Maisha yanatoa arufu nzuri iwapo yaantolewa kama zawadi na maisha hayana radha iwapo yanajificha yenyewe katika ubinafsi.

Baba Mtakatifu amesisitiza: somo la kwanza linaeleza ni mahali pa  kuchota hekima ya maisha, kwa maana anayetaka kujisifu  ajisifu katika Mungu. Kutambua Yeye na kukutana na Mungu ambaye anaokoa, anasamehe, ndiyo njia ya hekima. Katika Injili Yesu anasema “njooni kwangu ninyi mliochoka na kuelemewa na mzigo” (Mt 11,28), Je ni  nani anaweza kuhisi amebaguliwa kwa mwaliko huo? Je ni nani anaweza kusema mimi sina haja ya mahitaji?

Padre Pio alitoa maisha yake kwa idadi kubwa ya wanaoteseka ili waweze kukutana na Bwana na ndugu. Zana msingi ya kukutana ilikuwa ni sanduku la maungamo, sakramenti ya mapatano. Pale alianza maisha ya hekima, inayopaswa na kusamehe, hapo alianza uponyaji wa mioyo. Padre Pio alikuwa mtumishi wa  maungamo. Hata leo hii tunaalikwa, akiwa pale na kuuliza unakwenda wapi? kwa Yesu au katika huzuni yako: Je unarudi wapi? Kwa yule anayekuokoa au katika mapambano yako, majonzi na katika dhambi zako? Njoo Bwana anakusubiri. Kuwa jasiri hakuna jambo kubwa la kuzuia huruma yake. Makundi ya sala,wagonjwa wa hospitali,sanduku la maungamo ni vitu vitatu vinavyoonekana na ambavyo vinatukumbusha urithi wa thamani ya  sala, udogo na hekima ya maisha, na hivyo Papa Francisko amemalizia akimba neema ya kuvipalilia kila siku.


Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.