2018-03-16 17:30:00

Makuhani wawe na mahusiano kati yao na waongozwe na Roho Mtakatifu


Ni siku ambayo si rahisi kuisahau ya tarehe 16 Machi 2018 ambapo  Baba Mtakatifu amekutana na waseminari na mapadre wa Taasisi za Kipapa zilizoko mjini Roma. Katika mkutano huo kwenye ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI, wamejiandaa kwa nyimbo, sala na masomo ya tafakari kabla ya Baba Mtakatifu kuingia na alipoingia , wamempokea kwa furaha kubwa. Mara baada ya salam kutoka kwa Kardinali Beniamino Stella , Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Wakleri, wameanza mazungumzo na Papa Francisko ambapo amejibu maswali matano ambayo yalijikita zaidi juu ya mafunzo na tasaufi ya kikuhani kwa ujumla. Baba Mtakatifu ametoa wosia mzito kwa waseminari na wakleri katika lugha ya kawaida iliyosheheni mifano hai kabisa ya maisha ya kila siku.

Aliyesoma swali la kwanza alikuwa mseminari  kutoka Ufaransa  akiwakilisha watu wa Ulaya, ambapo ameulizwa ni jinsi gani ya kuweza kuweka pamoja shughuli za ukuhani kwa unyenyekevu wa kuhisi utume na umisionari. Akijibu swali hili anasema, padre anapaswa kuwa daimamtu ambaye yuko  katika mwendo , mwanaume wa kusikiliza lakini hasiwe kamwe peke yake: awe na unyenyekevu wa kutafuta wa kumsindikiza kiroho. Jambo msingi ni lile la kuwa na uwezo wa kung’amua ili kutambua namna gani ya kwenda mbele, kung’amua kile ambacho nisawa na kisichafaa. Amejibu hilo katika swali la pili lililosomwa na mwakilishi kutoka nchini Sudan, kuwakilisha Afrika.

Aidha Papa anasema kuna aina  mbili za kufuata ukweli wa mang’ammuzi; kwanza anayesali, mbele ya Mungu na kuweza kukabiliana na mwingine, yaani kiongozi mwenye uwezo wa kusikiliza na kutoa maelekezo. Iwapo hakuna mang’amuzi katika maisha ya padre, kuna hali ya kusimama na kujifungia binafsi kwa kufikiria kuwa na utakatifu lakini ambao haupo. Hakuna uwezo wa kwenda mbele. Yote yamefungwa, roho Mtakatifu hafanyi kazi. Papa amewahimiza mapadre kuwa na tabia ya kuomba Roho Mtakatifu  kama msindikizaji wa safari ya maisha. Ameongeza kusema kuwa wakati mwingine kuna hofu ya Roho Mtakatifu ukifikiria anataka kukufunga. Haitoshi kuwa wema tu bali kuishi kama vile Roho hayupo.

Swali la tatu kuhusu mafunzo ya kikuhani lilisomwa na padre kutoka Mexco ,ameomba Papa jinsi gani ya kuweza kuwa na uhusiano  kamili wa kikuhani kwa kipindi  cha mchakato wa maisha yake. Papa anasema ni lazima kuwa watu wa kawaida, binadamu, mwenye uwezo wa kufurahi na wengine, kucheka wakati mwingine, kusikiliza katika ukimya na kutoa maisha kwa wengine. Padre si mtu kama aliye ajiliwa kazi takatifu au aliye ajiliwa na Mungu.

Na swali la nne kuhusu tasaufi ya padre wa kikuani; swali hilo imesomwa na shemasi kutoka Marekani akitaka kujua tasaufi ya padre wa jimbo , kwa maana nyingine ambaye ajihusishi na mafundisho ya mwanzilishi au mwingine. Papa amejibu kwa neno moja (diocesanita’) akiwa na maana kuwa "ujimbo"… hivyo anasema, padre anapaswa kutunza mahusiano na Askofu wake, hata kama ni aina ya mtu mgumu,padre lazima  kuwa na mahusiano na ndugu mapadre , na waamini wa parokia ambao ni watoto wake. Ameongeza kusema, iwapo watafanya huduma yao katika kitovu cha mambo hayo matatu kwa hakika watakuwa watakatifu.

Swali la mwisho na la tano lilikuwa linahusu juu a mafunzo ya kudumu ya padre, lilosomwa na padre kutoka Ufilippini akiwakiliosha bara la Asia. Papa amewashauri kutunza majiundo yao vema hasa kwa kipindi hiki., bila kupoteza fursa maana hawatapata fursa hiyo: Majiundo hayo yanawasaidia kama ya kibinadamu, kichungaji, kitasaufi  na kijumuiya. Mafunzo ya kudumu anasema, yanatokana na utambuzi wa dhamiri ya udhaifu binafsi.  Ni muhimu kutambua udhaifu binafsi, anathibitisha. Hata hivyo akizungumza zaidi anasema kuwa mafunzo hayo wakati huo yameingilia na utamaduni wa sasa, kwa mitandao ya kijamii na hivyo ni lazima kujiuliza jinsi gani ya kuishi mawasiliano ya mitandao ya kijamii, jni insi gani ya kutumia simu za mikononi binafsi Aidha kujiandaa kukabiliana na changamoto za vishawishi ambavyo vijakuja juu ya usafi wa useja na mwisho kujitazama zaidi juu ya majivuno, kupenda fedha, ukubwa hata mambo ya anasa!

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News. 








All the contents on this site are copyrighted ©.