2018-03-15 15:28:00

Papa Francisko: Majadiliano mubashara kati ya Mungu na Musa!


Ujasiri na uvumilivu katika maombi ni msingi unaopaswa kuwa nao ili kuupeleka kwa Mungu ukiwa uhuru kama mwana wake. Ni maneno ya Papa Francisko wakati wa mahubiri ya asubuhi tarehe 15 Machi 2018, katika Kikanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Papa Francisko ameanza takafakari yake akiongozwa na somo la kwanza kutoka kitabu cha Kutoka, mahali ambapo Mungu naongea na Musa kuhusu watu wake waliojiharibu  nafsi zao.(Kut 32:7-14). Nabii anatafuta kila njia ili kuwaokoa watu na hasira aliyo nayo Mungu juu ya watu hao, ambao wameacha utukufu wa Mungua hai na kujitengenezea miungu ya dhahabu. Katika mazungumzo hayo Musa anamkaribia kwa majadiliano kwa kumkubusha mbali ya mambo aliyowatendea hasa ya kuwaokoa kutoka utumwani Misri,hata kufikia kumbukumbu ya uaminifu wa Babu Ibrahimu na Isaka. Katika maneno yake uso kwa uso, Musa anaonesha ni jinsi gani alivyo na upendo mkuu wa dhati kwa watu wake.  Musa haogopi kusema ukweli, yeye hana mchezo wa mantiki ya ufisadi, hata kuangukia kwenye kigezo cha kuwa na uwezo ili kuuza dhamiri yake.  

Kwa hali ya hiyo, inampendeza Mwenyezi Mungu, anasisitiza Papa; na  kwamba Mungu daima anatazama ndani ya roho ya mtu anayesali sana bila kuchoka  kwa ajili ya kutafuta kitu,anaye Sali hadi kufikia kuamsha moyo wa huruma ya Mungu.  Hakuna rushwa na ufisadi. Kwa maana Musa yuko na watu wake tu. Papa Francisko anasisitiza, hiyo ndiyo sala ya kuomba, sala ya mazungumzo ambayo ni ujasiri wa kuongea uso kwa uso na Bwana, sala ya uvumilivu kwa maana inahitaji uvumilivu katika sala. Aidha anaonya kuwa, haiwezekani kutoa ahadi ya kusali kwa ajili ya mtu alafu ukaishia kusema, Baba Yetu na Salam Maria basi. Hapana! badala yake iwapo umetoa ahadi ni lazima kupitia njia hiyo ya ujasiri na uvumilivu, kwa maana inahitaji uvumilivu katika maombi!

Katika maisha ya kila siku kwa bahati mbaya Papa naasema zipo kesi nyingi,hasa za baadhi ya wakuu wa makampuni kuamua kufunga kampuni kwa ajili ya kuokoa shughuli zake binafsi au kupata faida. Lakini Musa hakufanya hivyo, wala kuingia katika mantiki hiyo ya ufisadi, yeye alikuwa na watu na alipambana kwa ajili ya watu wake. Katika maandiko matakatifu yamejaa mifano kama hiyo ya kuomba bila kuchoka, kuwa na ujasiri na uwezo wa kwenda  mbele kwa uvumilivu katika sala  kama alivyo fanya mwanamke mkananea, na kipofu aliyeshuka bondeni mwa Yeriko. Katika maombi  kuna ulazima wa  kuwa na ujasiri, kusali bila kuchoka na uvumilivu. 

Iwapo unataka Bwana asikilize kile unachokiomba ni lazima kuendelea kuomba bila kuchoka, kubisha mlango hadi mlango wa moyo wa Mungu bila kuchoka kwasababu moyo una jali na kutambua kuile ambacho unahitaji. Lakini iwapo moyo haujihusishi zaidi na mahitaji hayo, kwa mtu ambaye ninapaswa kumwombea, siyo rahisi kuwa na ujasiri na uvumilivu. Kwa maana hiyo, Papa Francisko anasisitiza juu ya kuguzwa moyo katika sala kwa maana njia ya sala ya maombi ni lazima kuguswa zaidi, kupambana, kwenda mbele na kufunga. Amehitimisha akiomba neema hiyo hasa tunaposali mbele ya Mungu kwa uhuru kama watoto wake. Tusali bila kuchoka, tusali kwa uvumilivu, na zaidi kusali kwa utambuzi wa kuwa, ninazungumza na Baba yangu anaye nisikiliza. Na Bwana atusaidie kuendelea mbele kwa kusihi katika maombi hayo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.