2018-03-14 15:51:00

Papa amekutana na wawakilishi wa dini ya Utao kutoka Taiwan


Tarehe 14 Machi 2018  asubuhi, masaa ya Ulaya, Papa Francisko amekutana na kusalimiana na wawakilishi wa dini ya Utao kutoka Taiwan katika ukumbi mdogo wa mikutano wa mwenye heri Paulo VI. Wakati wa kutoa neno bila maandishi, amewashukuru ujio wao na kwa maneno ya hotuba yao. Aidha ameshukuru shughuli ya pamoja ya Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya kidini. 

Papa Francisko akizungumzia juu ya majadiliano ya kidini amesema, Mazungumzo yanakuwa ni majadiliano, iwapo mawazo ya mazungumzo hayo ni ya kibinadamu na  kutoka kwa watu ambao wanasaidia kukua wote  kwa kujikita katika njia moja za kutafuta Mungu wa kweli aliye wa pekee. 
Kadhalika amewashukuru sana kwa mapenzi yao mema, ya kufanya matembezi hayo na hata kuwashukuru sana kwa  mwaliko wao walio mpatia ili atembelee huko Taiwan.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.