Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Mandalizi ya Ziara ya Papa huko San Giovanni Rotondo yapamba moto!

Waamini wa San Giovanni Rotondo wanamsuburi Papa Francisko kwa hamu kubwa tarehe 17 Machi 2018 - ANSA

14/03/2018 16:05

Katika ziara ya Papa Francisko ya kuelekea Pietrelcina na San Giovann Rotondo mwisho wa wiki hii,mwandishi wa habari wa Vatican News amehojiana na Askofu Mkuu M. Castoro wa Jimbo Kuu Manferdonia-Veste–San Giovanni Rotondo kuhusu maandalizi ya waamini kwa kumpokea Papa Francisko, pia juu ya mkesha wa vijana wa San Giovanni Rotondo kwa ujio wake. Askofu Mkuu anasema, katika maparokia mbalimbali siku zilizopita wamefanya maandalizi hayo na baadaye wanatarajia pia kufanya mkesha kwa ajili ya kuombea ziara ya Papa. Maandalizi hayo yanafanyika katika liturujia zote na matukio mengi ya kiutamaduni, kwa kutafakari juu ya utume wa Papa na kutathimini ishara zake nyingi za upendo, kwa sababu, Papa Francisko  leo hii ni kiungo msingi cha habari mpya,hata kwa maono ya pamoja ya kiutamaduni anathibitisha Askofu Mkuu Castoro. Na akizungumza juu ya sura ya Mtakatifu Padre Pio, anawezaje kusaidia binadamu wa leo kufikia Kristo, Askofu Mkuu Castoro anafafanua kuwa, Padre Pio alikuwa ni mtu wa maana katika maisha ya wengi.  Na ndiyo maana unaweza kutambua pia jinsi gani Papa Francisko anapenda sura hii ya Mtakatifu Padre Pio.

Enzi za Padre Pio alikuwa amezungwa na watu wa dunia kama vile wanasanii, wana michezo, hata kisiasa, wote walikuwa wanakwenda San Giovanni Ritondo kukutana na Padre Pio, japokuwa yeye alikuwa kama vile mtumwa yaani kuwa mbali ya kukaribia ulimwengu wa namna hiyo. Mara nyingi Padre Pio alitoa jibu wazi, kwa yule aliyefika akipmea neema kutoka kwake ya kwamba, yeye atengenezi neema, anayetoa neema ni Bwana. Padre Pio alikuwa akijibu kuwa, yeye alikuwa ni fratelli mnyenyekevu na mtii anayesali, pia kuongeza kusema; atasali kwa ajili ya huyo aliye omba neema.

Askofu Mkuu Castoro anathibitisha kuwa, ndiyo mantinki msingi hasa ya Padre Pio ambaye inaweza kufafanuliwa kwa aina mbili: mantiki ya sala na ya upendo kwa ndugu. Yeye alikuwa ni mtu wa sala, aliyetambua kusali asubuhi na jioni wakati huo huo alikuwa anaungamisha masaa yote kwa siku. Halikadhalika kutambua jambo msingi la kuanzisha nyumba ya mateso, ambayo kwa sasa kimekuwa ni kituo kikubwa cha kupokea wagonjwa, si wa Italia tu bali hata Ulaya na maendeo mengine ya dunia. Ikumbukwe kuwa, ziara ya papa Francisko ya kwenda Pietralcina na San Giovanni Rotondo inatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 17 Machi 2018, mahali ambapo atatembelea sehemu alizoishi Padre Pio kwa sababu ya tukio la kumbukumbu ya miaka 100 tangu alipopata madonda(1918) na miaka 50 tangu kifo chake. Kwa maana hiyo furaha ni kubwa sana kwa waamini na maelfu ya mahujaji wanaosubiriwa huko San Giovanni Rotondo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

14/03/2018 16:05