Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Katekesi ya Papa kuhusu Misa Takatifu:Komunio na Sala ya Baba Yetu!

Papa Francisko katika katekesi yake ameelezea juu ya Ekaristi na sala ya Baba Yetu

14/03/2018 15:24

Katika karamu ya mwisho, Yesu mara  baada ya kuchukua mkate na kikombe cha diva na kushukuru Mungu,  tunatambua ya kwamba aliumega mkate. Tendo hilo linafanana na lile la Liturujia ya ekaristi katika Misa katika kuumega mkate na baadaye kufuata sala aliyotufundisha Bwana, yaani Baba Yetu”. Huu ndio utangulizi wa tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko, wakati wa mwendelezo  wa kateksi ya kila Jumatano kuhusu Ibada ya Misa Takatifu Tarehe 14 Machi 2018 katika viwanjia wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea kuelezea sehemu hiyo anasema kuwa, katika  maandalizi ya kumunio, ni sehemu ya kutoa sifa na maombi ya sala ya ekaristi na kusali sala ya Baba Yetu. Lakini hiyo  si aina  mojawapo ya sala zilizo nyingi za kikristo, bali ni sala ya wana wa Mungu na ndiyo sala kubwa! Ni sala ambayo tulifundishwa na Yesu yaani Baba Yetu. Kwa hakika katika kukabidhiwa siku ya Ubatizo wetu, sala hiyo inajikita katika hisia sawasawa na zile za Yesu Kristo. Sisi tunaposali sala ya Baba Yetu, tunasali kama alivyo lali Yesu mwenyewe. Ni sala ambayo Yesu aliomba na kutukabidhi; Mitume waliomba Mwalimu tufundishe kusali kama unavyo sali wewe, Yesu alikuwa akisali hivyo; ni jambo jema kusali kama Yesu!

Kwa mwaliko wa mafundisho yake, tunaweza kumwelekea Mungu kwa kumwita Baba kwasababu tumezaliwa kama wana wake kwa njia  maji na Roho Mtakatifu(taz Ef 1,5). Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. (cfr Rm 8,15. Lakini tunapaswa kufikiria kuwa hakuna awezaye kuita Baba iwapo hauna shauku ya Roho, Baba Mtakatifu anathibitisha!

Lakini je ni mara ngapi watu wanasali Baba Yetu,hawajuhi nini wanasema. Je unatambua kuwa ni baba yako, ni baba wa binadamu na baba wa Yesu Kristo? Je unao uhusiano na Baba? Tunaposali sala ya Baba Yetu ni lazima kuunganisha na Baba ambaye anatupenda  vilevile ni Roho ya kutuunganisha na hisia hizo za kuwa wana wa Mungu anathibitisha Papa Francisko. Je, ni sala gani iliyo bora zaidi ya hiyo, ambayo Yesu ametukabidhi  katika sakramenti ya komunio na Yeye? Hakuna zaidi! Na zaidi katika Misa, sala ya Baba Yetu inafanyika asubuhi na jioni, katika masifu ya asubuhi na jioni kwa maana ni wana wanao mwelekea Mungu na kindugu, pamoja na jirani ili kuchangia kutoa muundo wa kikristo katika siku zetu. Katika sala ya Bwana, hasa Baba Yetu, sisi tunaomba mkate wa kila siku kwa namna ya pekee katika Mkate wa ekaristi ambao tunahitaji ili kuishi kama wana wa Mungu. Tunaomba hata kuondolewa makosa yetu ili kustahili kupokea msamaha wa Mungu na kujitahidi kuwasamehe wangine wanao tukosea.
 
Baba Mtakatifu lakini nasema hiyo siyo rahisi, kwasababu kusamehe waliotukosea, ni neema ambayo lazima kuomba kwa Mungu na kusema: Bwana nifundishea kusamehe kama wewe ulivyo nisamehe mimi. Kwa nguvu zetu Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha siyo rahisi, bali ni kwa njia ya neema ya Roho Mtakatifu tunaweza kusamehe. Na tukiwa tayari kufungua mioyo kwa Mungu, Baba Yetu yuko yayari kutoa hata upendo kindugu. Mwisho tunaomba kwa Mungu atuondolee mabaya ambayo yanatutengenisha na yeye hata ndugu. Ni utambuzi wa dhati ambao unasaidia kujongea meza yake ya Komunio Takatifu.

Wakati wa sala ya Baba Yetu ikiendelea, ipo sala ambayo inatolewa ya na Padreakwa jina la wote: utukuo ee bwana na maovu yote na kutujalia amani katika siku zetu. Baadaye inafuata sehemu ya amani. Lakini kabla yake, ni kusali kwa Kristo ambaye ndiye zawadi ya amani (taz Yh 14,27), katika ulimwengu; hii ni kitu kingine ambacho Yesu anatenda ili Kanisa likue katika umoja na amani kwa mujibu wa matashi yake na hivyo ipo ishara ya kubadilisha amani kati yetu kuonesha umoja wa Kanisa na upendo kindugu , kabla ya kupokea sakramenti.

Sehemu ya kupeana amani, iliwekwa tangu zamani kabla ya kupokea kumunio. Na kwa mujibu wa ushauri wa Mtakatifu Paulo, haiwezekani kupokea tu mkate ambao unatufanya tuwe Mwili wa Kristo bila kujua kwa dhati upendo wandugu. (taz 1 wakorinto10,16-17; 11,29).(  Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?  Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

Amani ya Kristo haiweze kuchimba mizizi katika moyo usio kuwa na uwezo wa kuishi kindugu au kuishi baada ya kusababisha majeraha. Amani inatoka kwa Bwana.Hata Bwana anatupatia neema ya msamaha kwa wale wanaotukosea. Ishara ya amani inafutia kuumega mkate, tendo ambalo tangu mwanzo mitume walitoa jina la maadhimisho yote ya Ekaristi. Ni tendo lililotimizwa na Yesu ambalo baadaye liliwaruhusu mitume kumtambua mara baada ya ufufuko wake. Kumbuka mitume katika njia ya Emmau, walizungumza na mfufuka, lakini wakamtambua mara baada ya kuumega mkate na kutoweka. (taz Lk 24,30-31.35).

Tendo la kuumega mkate wa ekaristi, linasindikizwa na maombi ya Mwanakondoo wa Mungu: huo ni ushuhudua kuoka kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji aliyowalekeza wafuasi wake kumtazama Yesu mwana kondoo anayetoa dhambi za dunia    (Gv 1,29). Ni ishara ya kibiblia inayozungunza juu ya ukombozi (Taz Es 12,1-14; Is 53,7; 1 Pt 1,19; Uf 7,14). Katika kuumega mkate wa ekaristi, kwa ajili ya maisha ya dunia, waamini katika sala wanatambua mwanakondoo wa kweli wa Mungu ambaye ni Kristo mkombozi na kusema utuhurumie na utujalie amani”. Utuhurumie na utujalie amani, maombi ambayo yapo katika sala ya Baba Yetu na katika kuumega mkate, inatusadia kuweka nafsi zetu kishiriki kikamilifu katika ekaristi, kisima cha umoja na Mungu na ndugu wote.  Baba Mtakatifu amemalizia katekesi yake, akikumbusha kutosahu sala kubwa ambayo Yesu mwenyewe alitufundisha yaani sala ambayo yeye alikuwa akisali na hivyo amewataka wote kusali sala hiyo kila mmoja kwa kimya katika lugha zao.

Sr Angela Rwezaula.
Vatican News.

14/03/2018 15:24