Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Mtumishi wa Mungu Kardinari Elia !

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alihutubia huko Vincenza Italia wakati wa sherehe za heshima ya Mtumishi wa Mungu Kard. Elia Dalla Costa - REUTERS

14/03/2018 16:24

Tarehe 13 Machi 2018 jioni huko Vincenza nchini Italia Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican alitoa hotuba yake katika Taasisi ya Masomo ya juu ya Sayansi ya Dini  kwa mantiki kubwa katika  mpango wa kutoa heshima ya Kardinali Elia Dalla Costa ambaye ni mtumishi wa Mungu aliyekubaliwa hivi karibuni kutangazwa kuwa mwenye heri. Akianza hotuba yake, ameshukuru mwaliko kutoka jimbo la Vincenza  ili naye kushiriki  kutoa heshima ya Kardinali Elia Dalla Costa ambaye miezi michache iliyopita ameweza kutambuliwa fadhila  za utakatifu kati ya watakatifu wa Kaninsa kwa uthibitisho wa Baraza la kipapa la kuwatangaza watakatifu tarehe 4 Mei mwaka jana na Baba Mtakatifu ambapo kwa sasa ni Mwenye heri.

Kardinali Dalla Costa, anasema amejivunia katika Kanisa la Firenze, mahali ambapo alifanya kazi ya kichungaji tangu mwaka 1931-1958. Uthibitisho wa Papa ni msingi kwa ajili ya utambulisho wa maisha na matendo ya Kardinali Dalla Costa kwa namna ya pekee huduma yake kwa watu wa Firenze na ushuda wa hali ya juu katika tasaufi ambayo inaangaza shughuli nzima ya uchungaji mwema ulioweza kutolewa katika majimbo, pia katika kutetea hadhi ya watu wakati wa majanga ya vita na kuteseka kwa ubaguzi wa rangi kwa upande wa wayahudi.

Kardinali Parolin anashukuru kwa mwaliko huo wa Askofu Beniamino na kwa wote walioandaa Mkutano huo kwasababu, Kardinali Dalla Costa,  kwa upande wake amekuwa sura msingi ambayo aliiipenda sana tangu utoto wake.  Amesimulia wakati alikuwa mtoto alisikia hisotia yake kutoka kwa baba yake mdogo ambaye mara baada ya kuo alihamia na kuishi huko Pozzoleone. Alisimulia historia yake kwa  shauku kubwa hasa ile ya kusema alikuwa ni padre mtakatifu,  na ambaye aliacha mengi katika mioyo ya wanaparokia, nahadi sasa  baada ya miaka 50 bado anakumbuka hisotria hiyo. Zaidi sura ya Kardinali, imetambuliwa kwa njia ya  maandishi yake na historia  yake kupitia vitabu vya waandishi mbalimbali,akitaja Tito Casini kilicho andikwa huko Firenze mwaka  1972.

Kardinali Parolin anasema ni kutabu kilicho mvutia sana katika maisha yake, kama padre na kama askofu. Hata hivyo anathibitisha kuwa hadi sasa Kardinali Dalla Costa kwake yeye ni mfano wa kuigwa, na ndiyo maana anafurahia hata tarehe 13 Machi kwenda sambamaba mba na kuanzishwa kwa Taasisi ya Papa Pio XI mwaka 1933. Pamoja na kutaja mwandishi Tito Casini, lakini bado anasema kuwa wapo watafiti  wengi, vitabu na magezeti ambavyo kwa miaka mingi iliyopita hata sasa wameweza kufuatilia na kumpenda Mtumishi wa Mungu Kardinali Elia Dalla Costa. Kardinali Parolin alihitimisha hotuba yake, ili kuwachia ngazi wengine waendele  kuelezea zaidi juu ya maisha ya mtumishi wa Mungu Elia Dalla Costa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

14/03/2018 16:24