Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

Tanzia: Askofu Jean Bimenyimana wa Cyangugu, Rwanda amefariki dunia!

Tanzia. Askofu Jean Damascène Bimenyimana wa Jimbo Katoliki Cyangugu, Rwanda amefariki dunia. - ANSA

13/03/2018 10:50

Baraza la Maaskofu Katoliki Rwanda, linatangaza kifo cha Askofu Jean Damascène Bimenyimana wa Jimbo Katoliki la Cyangugu kilichotokea Jumapili tarehe 11 Machi 2018 kwenye Hospitali ya Kijeshi ya Kanombe, iliyoko Jijini Kigali. Itakumbukwa kwamba, Marehemu Askofu Jean Damascène Bimenyimana alizaliwa tarehe 22 Juni 1953 huko Shangi, Rwanda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 6 Julai 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Jimboni Nyundo na tarehe 5 Novemba 1981 akahamia na hatimaye akajiunga na Jimbo Katoliki la Cyangugu.

Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Cyangugu tarehe 2 Januari 1997 na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu akiwa na dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu Jimboni Cyangugu hapo tarehe 16 Machi 1997. Na tarehe 11 Machi 2018, akiwa na umri wa miaka 65 amefariki dunia!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Vatican News!

13/03/2018 10:50