Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Papa mstaafu Benedikto XVI kumwandikia Barua mons. Edoardo Viganò!

Monsinyo Vigano' wakati wa kusoma barua ya Papa mstaafu Benedikto XVI katika kuwasilisha vitabu Taalimungu ya Papa Francisko - RV

13/03/2018 16:45

Na tarehe 12 Machi 2018 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ameandika barua kwa Monsinyo Edoardo Vigano, kufuatia juu utoaji wa mfululizo wa vitabu juu ya “Taalimungu ya Papa Francisko”.

Monsinyo Vigano wakati wa kulezea juu ya Vitabu hivyo, anasema, Papa mstaafu Benedikto ametaka kutoa mchango wake kama kawaida, ikiwa na maana kubwa na  ili kuweka wazi umoja wa tasaufi ya ndani kati ya mapapa wote wawili. Barua yake binafsi ya Papa mstaafu Benedikto XVI juu ya mwendelezo wa utume wa Papa Fancisko aliyo mtumia  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican Monsinyo Vigano, yeye binafsi ameiweka  wazi wakati wa uwakilishaji wa vitabu hivyo ambavyo kwasasa vinapatika katika vitabu Vatican. Uwakilishaji wa vitabu hivyo umefanyaka jioni ya tarehe 12 Machi 2018 makao makuu ya Vatican News  chumba cha mikutano Marconi.
 
Katika barua hiyo, Monsinyo Edoardo Vigano anasema, Papa Benedikto anatoa sifa ya kuanzisha mtindo huo wa utoaji wa vitabu ili kutambua zaidi utume wa Papa Francisko katika dhana zote za kinadaria na matendo hasa katika mafunzo ya kitaalimungu au kifalasafa kwa ngazi ya maisha ya kikirsto leo hii.

Papa mstaafu Benedikto aidha anashukuru kupokea zawadi ya vitabu 11 vilivyo andikwa na wataalimungu maarufu  kimataifa. Na ambavyo vimehaririwa na Padre Robert Repole Mwenyekiti wa Taalimungu Italia. vitabu vidogo anaongeza, Papa Benedikto vinaonesha jinsi gani Papa Francisko alivyo mtu wa mafunzo ya kina kwa upande wa  kifalsafa na kitaalimungi na pia kusaidia kuona mwendelezo wa kina kati ya mapapa hao wawili pamoja na kuwa na tofauti ya mtindo na tabia zao.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

13/03/2018 16:45