Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Askofu Màrio Lukunde ang'atuka kutoka madarakani Jimbo la Menongue

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu Màrio Lukunge wa Jimbo Katoliki Menongue, Angola la kung'atuka kutoka madarakani. - AFP

12/03/2018 14:07

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Màrio Lukunde wa Jimbo Katoliki la Menongue, nchini Angola. Askofu mstaafu Lukunde alizaliwa kunako tarehe 13 Mei 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 3 Februari 1985 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kunako mwaka 2005 akamteuwa kuwa Askofu na hatimaye, kuwekwa wakfu hapo tarehe 9 Oktoba 2005. Tarehe 12 Mei 2018 Baba Mtakatifu Francisko akaridhia ombi lake la kutaka kung’atuka kutoka madarakani!

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwamba, Jimbo la Menongue, nchini Angola lina jumla ya Parokia 8 zinazohudumiwa na Mapadre 17 kati yao Mapadre wa Jimbo ni 14 na 3 ni Mapadre wa Mashirika ya Kitawa. Kuna watawa wa kike na kiume wapatao 46. Takwimu za mwaka 2015 zinaonesha kwamba, Jimbo lilikuwa na Majandokasisi 23.

Na Padre Richard A. Mjigwa. C.PP.S

Vatican News!

12/03/2018 14:07