Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich ni Mwenyekiti mpya wa Comece!

Askofu Mkuu Jean-Calude Hollerich wa Jimbo Kuu la Luxembourg amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Comece! - EPA

09/03/2018 15:01

"Sala ya kwa ajili ya kuiombea Ulaya ili kuondokana na kipindi hiki cha mvutano inayoongezeka kwa kila ngaza na mioyo iliyo jaa chuki na ukosefu wa matumaini,watu wa Ulaya na Taasisi za Umoja wa Ulaya zisiache kuendelea kutembea katika njia ya umoja na urafiki". Haya ni maneno ya Kardinali, Reinhard Marx, Askofu Mkuu wa Monaco na aliye malizia muda wake wa kama Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya, yaliyosikika katika Kanisa Kuu la Notre Dame du Dublo, katika moyo wa mji wa Bluxelles, hatua chache kutoka jengo la Makao Makuu ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Maaskofu wawakilishi kutoka Shirikisho la mabaraza ya maaskofu katoliki Ulaya wameunganika kuadhimisha misa kwa ajili ya kuiombea Ulaya, jioni ya tarehe 8 Machi 2018, mara baada ya siku maalumu kwa ajili yaComece! Maaskofu hawa wameunganika kwa pamoja katika mkutano wa mwaka ambapo wamemchagua mwenyekiti mpya Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich wa Jimbo Kuu Luxembourg na wasaidizi wake wanne, waliochaguliwa kwa  mantiki ya uwakilishaji wa maeneo yao  kama ifuatavyo: Askofu Noël Treanor (Ireland), Askofu  Mariano Crociata (Italia), Askofu  Jan Vokal (Jamhuri ya Uchek Cz) e Askofu Franz-Josef Overbeck (Ujerumani).

Katika mahubiri ya Kardinali Max amesema, kuwa ni kipindi cha kutafuta matumaini na ujasiri. Mungu ana mtazamo wa kila binadamu. Kwa maana ni baba wa watu wote waamini na wasio amini hivyo Kanisa linaalikwa kuwa chombo cha umoja kwasababu mahali palipo na chuki na ukosefu wa matumaini ni kama kuchimba shimo hivyo ni lazima kujenga madaraja ili kurudisha  hali halisi ya urafiki. 

Maaskofu wamefanya uamuzi wa kuzindua mwanzo wa Uenyekiti mpya wa Askofu Mkuu Hollerich, kwa maombi ya kuiombea Ulaya. Habari zinasema kuwa, katika Kanisa Kuu la Notre Dama wameombea hata viongozi wa kisiasa ili waweza kuongoza na hekima; kwa ajili ya maskini, amani duniani, kwa ajili ya nchi zilizo zenye vita, waathirika wa kila aina ya migogoro. 

Uchanguzi wa wa Askofu wa Jimbo Kuu la Lusemburg  kuwa mwenyekiti mpya wa shirikisho la Comece umefanyika ndani ya mkutano ulioanza tarehe 7-9 Machi 2018 huko Bruxellees .  Kwa mujibu wa Katiba yao, anabaki katika nafasi huyo kwa miaka mitano kuanzia 2018 kufikia 2013. Anashika nafasi ya Kardinali Reinhard Marx, ambaye ameongoza Comece kwa hawamu mbili ya miaka mitatu mitatu kuanzia ( 2012-2018). 

Wakati wa kutoa hotuba yake ya kwanza kama Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Maaskofu wa Ulaya amesema kuwa, yuko tayari kufanya kazi na watu wote wenye mapenzi mema ambao wanajikita kuheshimu na kulinda hadhi ya binadamu. Wakristo hawawakilishi kikundi  cha  manufaa yao binafsi, bali ni wazalendo wa Ulaya wanao jikita kwa dhati kujenga Ulaya na nyumba yao ya pamoja. 

Askofu Mkuu Hollerich ni mtu wa mazungumzo na  yeye ni mwanashirika wa Kijesuit. Tangu mwaka 1981 alijunga na Shirika la Yesu (Js)na kuendelea na mafunzo ya roho ya Kijesut katika Province ya Ubelgiji kusini na Lussemburg. Sehemu kubwa ya maisha yake ya kimisionari amekaa mjini Tokyo, ni mahali alipofunga nadhiri zake za milele katika Kanisa la Mtakatifu Ignatius.

Amefundisha Chuo Kikuu Katoliki cha Sophia mjini Tokyo na tangu mwaka 1999 alichaguliwa kuwa msimamizi wa Kanisa la Chuo hicho na baadaye kuchaguliwa kuwa Gombera wa chuo hicho. Tarehe 12 Julai 2011 Baba Mtakatifu msataafu Benedikto XVI, alimteua kuwa Askofu Mkuu wa Luxembourg. Hadi kuteuliwa kwake pia alikuwa ni mwenyekiti wa Mtandao wa Haki na Amani Ulaya, ni chombo ambacho kinaunganisha  zaidi ya Tume za kimatifa 30 chenye  lengo la  kuingilia kati katika mjadala wa umma juu ya masuala yanayohusu haki za kijamii, ujenzi wa amani na ulinzi wa mazingira.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

09/03/2018 15:01