2018-03-07 14:05:00

Kard.Piacenza:Ni marufuku Mapadre kuchat wakati wa Sakramenti ya Kitubio!


Katika maungamo ni sehemu ya kusikiliza na kukutana na Mungu, si mahali pa kwenda chumba cha maungamo na simu  imefunguliwa. Ni jambo ambalo halisitahili kubisa padre  kuungamisha wakati anatumia simu mkononi iwe, smartphone, iPad na jambo lolote la kiteknolojia ambalo linaweza kuhatarisha usikivu na umakini kwa Padre kwa muda mwafaka wa maisha ya mwamini anayeingia kujuta dhambi zake kwa Mungu. Ni suala ambalo halitoi ushuhuda kwa wote, hasa kwa upande wa vijana, pia ni kuondoa maana kamili na thamani ya sakramenti ya kitubio.

Ni tafakari ya Kardinali Mauro Piacenza,mhudumu Mkuu wa Idara ya Toba ya kutume akitoa tafakari tarehe 6 Machi katika mkutano  ulioanza tarehe 5 Machi  na utamalizka tarehe 9 Machi 2018. Idara hiyo  imeandaa mafunzo ya ndani ambayo yatahitimishwa kwa kukutana na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Machi 2018, siku ambayo pia ni maadhimisho ya Ibada ya Toba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican saa 11:00 masaa ya Ulaya.

Kardinali  Piacenza akiendelea na mafundisho hayo anathibitisha kuwa, zipo habari zinazosikika kutoka kwa waamini kuwa, kuna baadhi ya waungamishi wana chat wakati muungamaji anaendelea kutubu makosa yake. Hiyo ni hatari ambayo yeye binafsi anathibitishwa kuwa ni aina ya kumpinga Mungu kimatendo, na hali ya kuonesha udhaifu wa imani aliyo nayo muungamishi katika  tukio la neema kuu ya Mungu inayokuwa inaendelea kwa wakati huo. Vilevile anasema kuwa yapo  malalamishi kutoka kwa waamini wakilalamikia  baadhi ya mapadre waungamishi kukosa umakini na usikivu wakati wa mazungumzo na muungamaji, kwa mantiki hiyo, Kardinali Piacenza anatoa maelekezo kwa wote ya kukataza kutumia simu  katika chumba cha maungamo mahali ambapo ni tukio la sakramenti ya kitubio!

Akifafanua zaidi juu ya nini maana ya maungamo anasema: hawali ya yote ni usikivu wa hali ya juu kwa nyuzi 360. Na  zaidi ni mahali pa  makutano na Mungu na Kristo wa kweli;  Ni nafasi ya uhuru na fursa kwa ajili ya wito binafsi. Kwa namna hiyo tukio hili ni kwa ajili ya kuwasaidia waamini wote na vijana kwa namna ya pekee ili katika maungamo waweza kuonja  ule uzuri, ukweli na upendo utokao kwa Mungu.

Katika kitubio, mwamini analikwa kutambua uwazi wa moyo  wake, wakati wa kushiriki sakramenti ya mapatano na zaidi hasa kuwafikiria vijana ambao wanakaribia kitubio kwa uhuru wao. Hata hivyo  anabainisha kuwa, hadi nusu karne iliyopita, sakramenti ya kitubio  ilikuwa inafikiriwa mojawapo ya sakramenti ngumu kuliko zote na  hiyo ilikuwa inatokana na kasumba au hali ya kutoipenda na kuipinga. Leo hii lakini ni kinyume kwani kumekuwapo na utambuzi zaidi juu ya  huruma ya Mungu inayopatikana wakati wa kuijongelea sakramenti ya kitubio.Lakini pamoja na sababu hiyo muungamishi lazima awe na  tabia ya kuthamini anayekuja kuungama na kuonesha nini maana ya thamani ya kuungama dhambi na kujuta kupitia ishara ya kukaribia sakramenti ya kitubio.

Ili kuweza kutambua ni lazima kukubali misingi yake kwamba: Sakrameni ni matendo ya Kristo na Kanisa na kwa maana hiyo haiwezekani kuipunguzwa kamwe au   kuidhoofisha sakramenti hiyo katika maonesho ya imani binafsi, kama inavyotukia katika baadhi ya matukio ya kisasa. Ni tukio la aina ya pekee ya mapatano na watu walio mstari wa mbele mwamini nayeungama na padre muungamishi, kwa maana halisi anayeungama na Kristo mwenyewe.

Ili kufanikisaha hilo  Kardinali Piacenza  anawaomba waungamishi wote kuwa na ufahamu zaidi hata katika mantiki za kibinadamu wakati wa maungamo, hasa ile ya kuonesha upendo zaidi. Si wote wanakuja kuungama wanatambua kujeleza vema; wakati mwingine wapo baadhi  wanaingia katika maungamo wakijidai, na kwa maana hiyo inahitaji hekima na busara. Kwa kufanya hivyo itamsaidia zaidi anayeungama kutambua furaha iliyopo ndani msamaha  wa dhambi.

Kujihukumu binafsi dhambi mara nyingi ni tendo gumu, anathibitisha Kardinali Piacenza , kwani ni kujiweka mbele ya hukumu binafsi katika mawazo , maneno, matendo na kutotimiza wakibu. Ili kuweza kujihukumu binafsi inatakiwa nguvu ya Roho Mtakatifu, neema ya majuto kamili ambayo inaweza kugeuza maisha na kukutana furaha itokanayo na huruma ya Mungu!

Ni mkutano maalumu, ambao unaharibu dhambi na kukuacha huru. Anayeungama anatambua hili au labada hajuhi kuwa, kukaribia upatanisho wa Bwana unabadilisha maisha kamili . Kwa utambuzi huo kuna haja ya mapadre waungamishi kuwa na tafakari ya kina na Bwana ili kwamba muungamishi asiwe kizingiti cha yule anayekuja kuungma japokuwa inajilikana kwa walio wengi ya kuwa tendo la kuungama ni kama vile kukutana na hakimu na daktari.

Kardinali Piacenza   anasisitiza juu ya ukuu wa mazungumzo na mfumo mzima wa mapatano na Mungu kwa njia ya kitubio. Mazungumzo ndani ya kutubio  ni sehemu nyeti kwa pande zote mbili kwa maana zinahitaji usikivu,umakini, busara, uwezo wa kupokea kila hali hasa kwa upande wa mapadre ambao ni sehemu kuu inayowakilisha baba na ndiyo hatua ya kwanza ya muujiza wa mabadiliko anayo yafanya muungamishi.

Ni tunu msingi kwa binadamu anasema Kardinali Piacenza,na ndiyo ingekuwa inapaswa kuwa mstari wa mbele katika shughuli za kila wiki  kwa mfano Padre kukaa na kutafakari kwa kina juu ya namna ya kuungamisha. Kusali na kujiuliza maswali mengi  iwapo Padre anao uwezo  wa kusikiliza kwa makini na kuwa na utambuzi wa kuwa ni  kama baba katika maungamo!

Akifafanua j juu ya usikivu hasa akiwalenga vijana anasema kuwa na usikivu kwa vijana ni muhimu, maana katika nyakati zetu, usikivu kwa kizazi cha sasa umekuwa mdogo . Na ndiyo maana imechaguliwa Sinodi ya Maaskofu mwezi Oktoba kwa ajili ya Vijana ili kutembea nao kwa matumaini. Ni kutafuta namna ya kuwasiliana nao, kuwapokea , kuwa makini katika uwepo  wao kama binadamu wa leo na kesho na kutafakari uwezo wa vijana.Hiyo ni kwasababu wao ni sehemu msingi wa maisha endelevu ya jamii. Hata hivyo amekumbuka hata mfano wa mchangaji mwema kwa upande wa mapadre, ambapo amemkubuka Mtakatifu Maria Vianey, aliyekuwa padre na paroko wa vijijini na  mfano wa kuigwa katika maungamo.

Yeye alitambua kusikiliza watu wake na ikawa ndiyo kutambuliwa kwa kila mmoja . Yeye binafsi aliandika:“Mungu daima anasemehe, hata kama anatambua kuwa mwanadamu huyo atarudia  dhambi tena.  Siyo kusema kwamba kutenda dhambi ni haki, ni kutaka kuonesha kuwa dhambi ni udhaifu wa binadamu ambaye amejeruhiwa na dhambi ya asili kwa maana ya kuwa na akili, uhuru na utashi"

Sr Angela Rwezaula

Vatican News!
 








All the contents on this site are copyrighted ©.