Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Papa kutembelea Makao Makuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni

Tarehe 21 Juni 2018 Papa Francisko anatarajia kufanya ziara jijini Geneva katika Baraza la Kiekumene la Makanisa Ulimwenguni

02/03/2018 16:17

Papa Francisko anayo nia ya kutembelea Baraza la Makanisa Ulimwenguni katika  makao makuu yaliyoko huko Geneva kutokana na tukio la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Ziara yake inatarajiwa kufanyika  tarehe 21 Juni 2018. Hayo ni maelezo ya kwa mujibu wa Msemaji mkuu wa Vatican Dr. Greg Burke kwa waandishi wa habari, tarehe 2 Machi 2018 akifafanua pia kwamba, mpango nzima wa  Ziara yake ya kitume utatangazwa baadaye.

Vile vile tarehe 2 Machi 2018  katika chumba cha mikutano ya habari Vatican wamewakilisha kwa vyombo vya habari mipango yote inayohusu maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni. Kutokana na ziara hiyo Papa Francisko atakuwa Papa wa tatu kutembelea makao Makuu ya Baraza la kiekumene la Makanisa Ulimwenguni. Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea  tarehe 12 Juni 1984, akiwa katika ziara yake ya kichungaji katika Shirikisho la Makanisa ya huko Ulaya Kaskazini. Lakini kabla ya matembezi hayo  alitangulia hata Mwenye heri Papa Paulo VI tarehe 19 Juni 1969 miaka 4 baada ya kufunga Mtakaguso wa II wa Vatican.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

02/03/2018 16:17