Baba Mtakatifu Francisko kama kawaida ya kila mwezi kutoa nia ya maombi, hata mwezi wa tatu ametoa nia zake kwa njia ya video akisema kuwa : katika enzi ambazo tunaishi , tunaalikwa kwa kina kuwa na uwezo wa kung’amua, yaani kung’amu kila aina ya sauti, ile sauti ya Bwana, sauti ambayo inatupeleka katika Ufufuko , katik amaisha na sauti ambayo inatukomboa dhidi ya kuanguka katika utamaduni wa kifo. Tuna haja ya kujitafiti dhamiri zetu , yaani kujua kitu gani ambacho Bwana anataka ili kuishi katika upendo na kuendelea katika utume wake wa upendo. Kwa njia hiyo tusali pamoja kwa ajili ya Kanisa zima ili litambue dharura ya mafunzo ya kung’amua kiroho na juu ya mpango binafsi na wa jumuiya.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©. |