Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Nyaraka

Barua ya Palacuit Deo inayohusu baadhi ya mantiki ya wokovu kikristo!

Barua ya“Placuit De” ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki inayohusu baadhi ya mantiki ya wokovu kikristo. - RV

01/03/2018 16:29

Barua ya“Placuit Deo” ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Maaskofu wa Kanisa Katoliki inayohusu  baadhi ya mantiki ya wokovu ya kikristo. Barua imetangazwa tarehe1 Machi 2018 ikiwa imeidhinisha na Papa Francisko na saini ya Askofu Mkuu, Luis Francisco Ladaria Ferrer,Mwenyekiti  wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Askofu Mkuu Giacomo Morandi,Katibu wa Baraza hilo. Kwa utangulizi wake inaanza: Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na urathi wake,aliokusudia katika yeye huyo. (taz Ef 19); Pt 1,4). [...] Maana ni kwa njia ya Yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Umungu, mkikombolewa kutoka uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

Mafundisho juu ya wokovu  Kikristo yanatakiwa daima  na kwa upya kutafakari kwa kina. Kwa kutazama juu ya upeo wa Bwana  na  Kanisa ambalo linajikita kwa upendo wa umama kwa watu wote, ili kuwatangazia wao ishara nzima ya Agano la Baba, ambaye kwa njia ya Roho Mtakatifu, anataka kuwapeleka kwake Kristo, mtawala mkuu wa mambo yote. (Ef 1,10).  Barua hii inataka kuonesha bayana Katia ukuu wa utamaduni wa imani na kwa namna ya pekee juu ya mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko, baadhi ya mambo ya wokovu  kikristo ambao leo hii  unaweza kuwa mgumu kutambua kutokana na mabadiliko ya utumaduni.

Ni kutokana na matukio ya sasa na mabadiko ya utamaduni juu ya maana ya wokovu kikristo, ulimwengu mambo leo  unahisi kwa shida kubwa kukiri imani yake kikristo ambayo ilitangazwa na Yesu mkombozi wa mtu na binadamu wote (taz. At 4,12; Rom 3,23-24; 1 Tm 2,4-5; Tit 2,11-15). Kwa upande mwingine ubinafsi umeingilia suala la kutaka kujitosheeleza, suala linalo mzingira binadamu anayefikiria  kujitosheleza kwake kunategemea nguvu zake binafsi. Katika maono hayo, sura ya Kristo ambaye  ni mfano wa kuigwa kwa matendo ya ukarimu wake, maneno yake na ishara zake, haviwezi tena kwake kubadili hali ya maisha, katika kujinyenyekeza ndani ya  maisha na mapatano na Baba kati yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu (taz. 2 Cor 5,19; Ef 2,18).

Na kwa upande mwingine, upo usambaaji wa maono ya wokovu wa kina ambao unatoa nguvu ya kujiamini binafsi  au kutambuliwa hisia za kuunganika na Mungu, lakini bila kuwajibika na kuanza upya mahusiano yetu na wengine na dunia iliyoumbwa. Kwa mtazamo huo inakuwa vigumu kupokea maana ya Neno lililofanyika mwili na Yeye akajifanya kuwa sehemu ya familia ya binadamu na kuchukua mwili katika historia yetu na  kwa ajili yetu wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu!

Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake wa kawaida daima amekuwa akizungumzia juu ya tabia hizi ambazo zinawakilisha mienendo miwili iliyotajwa na ambayo inafanana na mantiki mbili za kizamani, zilizokuwa zikipinga dini na Mungu ( yaani pelagianism na Gnosticism). Katika nyakati zetu, inajirudia tabia ya “pelagianism” tabia ambayo inajikita hasa katika ubinafsi, wenye kuwa na mzizi wa kujitosheleza, kujidai kujiokoa binafsi bila kutambua kuwa kuishi kwake kunategemea na wengine, yaani uwepo wa Mungu na wengine kwa kina. Katika hali hiyo wokovu unajikabidhi katika hali hiyo na nguvu za mtu mmoja, au katika ujenzi wa kibinadamu tu,asiyekuwa na uwezo wa kupokea mapya ya Roho wa Mungu.

Na kwa upande wa aina nyingine ya kizamani ya kukana dini na Mungu yaani (pelagianism) mtu wa namna hiyo  anajiwakilisha katika kutafuta wokovu wa ndani, lakini uliofungwa ndani yake. Huo unajikita katika kujikweza na kujiona kuwa na akili zaidi ya mwili wa Yesu katika  fumbo la Mungu asiyejulikana. Anajidai kujiokoa yeye binafsi kwa kujikita ndani ya mambo ya ulimwengu, mahali ambapo hawezi tena kugundua hata chembe ya makutano wa Muumbaji, bali mbele yake anaona hali halisi na ukosefu wa maana na kuendelea kuishi kwa kujitambulisha, akifanya kuutumia utu wa binadamu kwa manufaa yake binafsi.  Ni wazi kwa upande mwingine kuona kuwa aina zote hizo mbili za wakana Mungu  (pelagianism na Gnosticism) ni kutaka kuonesha kuwa mantiki zao zina fanana,bila kuingilia hatari ya  imani katika biblia.

Binadamu anatambua moja kwa moja ua kinyume kuwa ni fumbo: kwa maana ya kujiuliza “Mimi ni nani, japokuwa sisitahihili ndani mwangu kuishi? Kila mtu kwa namna yake anatafuta furaha na anajaribu kuifuatilia katika hatua za mchakato wa  rasilimali alizo nazo. Licha ya tamaa hiyo ya ulimwengu siyo lazima kuielezea au kuitangaza; badala yake ni siri zaidi iliyojificha kiasi cha kuweza kuonekana na ipo tayari kujionesha mbele kwa namna ya pekee katika  dharura. Mara nyingi siri hiyo imejionesha katika matumaini ya afya ya mwili, wakati  mwingine inachukua umbo la wasiwasi kwa kiasi kikubwa katika usitawi wa uchumi, mara nyingine inajieleza wakati wa mahitaji ya amani ya ndani  na utulivu wa kuishi na jirani; Kwa upande mwingine, swali juu ya wokovu linajitokeza  kama shughuli kwa ajili ya wema mkubwa ambao unatunzwa hata kwa tabia ya kuvumilia na kushinda uchungu. Katika mtazamo wa kutafuta wema, pembeni mwake yapo  mapambano dhidi ya ubaya, unaosababishawa  na ujinga,makosa, udhaifu, magonjwa na kifo.

6.Kwa mtazamo wa shauku hizi za imani katika Kristo, tunafundishwa kukataa kila aina ya kujidai na kutaka kujitosheleza wenyewe; na kwamba tunaweza kuwa wakamilifu wa kweli iwapo Mungu mwenyewe anaweza kutuvutia kwenda kwake. Wokovu mtimilifu haupo katika mambo ya kibinadamu na ambaye anafikiri kujiponya  mwenyewe, kama vile kutawala mabaya au ustawi wa mambo, sayansi, teknolojia, uwezo au kutawala wengine , umaarufu au kujipendekeza. Hakuna kiumbe yoyote  anayeweza kujitosheleza, kwasababu Mungu ametuweka tuwe na muungano na Yeye na moyo wetu hauwezi kupata utulivu hadi kupumzika kwake”. Wito wa mwisho wa mtu kwa dhati ni mmoja ule wa umungu . Maonesha kwa namna hiyo hayana kizingiti cha kutangaza wokovu kama jibu linalotarajiwa wakati huu. Iwapo wokovu unaweza kuwa kinyume , kuhukumiwa au kupimwa kwa mujibu wa mahitaji ya kila kiumbe kinachoishi, inawezekanaje kuepuka tetesi rahisi za uumbaji wa Mungu Mwokozi aliyetufanya kwa sura ya mahitaji yetu?

7. Zaidi ni lazima kusisitiza kuwa kwa mujibu wa imani ya kibiblia , asili ya ubaya haipatikani katika ulimwengu wa mambo na mwili, au uzoefu kama kizingiti au kama magereza tunamotakiwa kukombolewa. Kinyume chake ni kwamba imani iliyotangazwa katika dunia nzima ni neema kwani tumeumbwa na Mungu (taz. Mw 1,31; Hek 1,13-14; 1Tim 4,4), na  kwamba ubaya unao muharibu mtu zaidi ni ule tuokao ndani ya moyo wake (taz. Mt 15,18-19; Mw 3,1-19)!. Binadamu anaptenda dhambi anaache chemichemi ya upendo na kupoteza umbo hilo la upendo ambao umefungwa daima ndani yake mwenyewe. Utengenisho huo na Mungu  ambaye ni kisima cha muungano na maisha na kupoteza  umoja kati ya watu na watu katika dunia, ndipo unaingia utawala mwingine katika ulimwengu  wa dhambi na mauti; hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;(taz. Rom 5,12). Matokeo ya wokovu ni kwamba imani uliyotangazwa haitazami historia ya ndani tu, bali mtu mzima. Kwa hakika mwili na roho vyote vimeumbwa kwa upendo wa Mungu na sura na mfano wake mwamandamu hiyo  anaitwa kuishi na muungano na Yeye.

8. Kristo , Mkombozi na Wokovu:Hakuna kipindi chochote cha hatua za binadamu ambacho Mungu ameacha kutoa wokovu kwa watoto wa Adam (taz. Mw 3,15);Yeye alifanya agano na watu wote kwa njia ya Nuhu (taz. Mw. 9,9) na mbele zaidi kwa  Ibrahim na uzao wake (taz. Gen 15,18). Wokovu wa Mungu  unajikita kwa namna hiyo katika uumbaji kwa kushirikisha watu wote  na kujikita katika hatua za safari ya dhati ya historia. Kwa kuchagua watu, ambao walitoa zawadi  kwa njia ya kupambana dhidi ya dhambi na kuweza kumkaribia; Mungu aliandaa kuja kwa Mkombozi mwenye nguvu , katika nyumba ya Daudi mtumishi wake (Lk 1,69). Katika utimilifu wa nyakati, Baba alimtuma Mwanae duniani, ambaye alitangaza ufalme wa Mungu na kuponya kila aina ya magonjwa(taz. Mt 4,23).

Uponyaji  uliotolewa na Yesu, ambao ulionesha uwepo hai wa Mungu na ilikuwa ni ushara ya kutuma mtu kwa niaba yake ambaye  aliwakilisha na kuonesha jinsi Bwana wa maisha alivyo, na kifo katika tukio la Pasaka. Kwa mujibu wa Injili, wokovu kwa watu wote ulianza  kupokelewa kwanza na Yesu. “Leo wokovu umefika nyumbani humu, “ ( Lk 19,9). Habari njema ya wokovu ina jina na sura; Yeye ni Kristo Mwana wa Mungu Mwokozi. Na mwanzo wa kuwa mkristo  hauna uamuzi  wa maadili au mawazo makubwa, bali ni kukutana na tukio yaani Mtu, ambaye anatoa maono ya maisha na mwelekeo mmoja; mwelekeo halisi!

9. Imani ya kikristo  katika karne nyingi za utamaduni, imejionesha kwa njia ya sura mbalimbali, na hasa, kazi ya wokovu wa Mwanae aliye jifanya mtu. Alifanya hivyo  kwa  mantiki timilifu, ambayo Kristo ametukomboa katika dhambi na kutukweza juu; Mwanae anatufanya tuwe wana wa Mungu na kushirikia asili ya Mungu kwasababu hiyo  “Tena  ametukirimia ahadi kubwa mno za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washiriki wa tabia ya umungu (taz. 2 Pt 1,4). Kwa kufikiria mtazamo wa wokovu maana tangu kuja kwa Mungu mwana kukombowa watu wake; Yesu ni mwanga, ni kiongoizi, mkombozi na mtoa huru na pia nayetaka kumtakasa kila mtu na kumpa haki yake.

Katika mtazamo wa utirhi  ( kutoka kwa watu kuelekea kwa  Mungu) Yeye ni Kuhani mkuu wa Agano jipya, anatoa sadaka kwa Bwana, kwa jina la watu, liturujia timilifu; anajitoa sadaka kwa ajili ya kutuondolea dhambi, daima ni hai  kutuombea sisi. Kwa namna hiyo jionesha  katika maisha ya Yesu maana  ni mkakati wa nguvu ya Mungu na mkakati wa kibinadamu ambaye ni msingi kwa mtazamo wa aina yake.  Kwa upande mmoja kushuka toa jii ni ushuhuda wa kwanza kabisa wa matendo ya bure ya Mungu; na unyenyekevu wa kupokea zawadi ya Mungu, kabla ya sisi kufanya kazi,  ni msingi ili kuweza kujibu ule upendo unao okoa. Kwa upande mwingine, maana ya kushuka juu ni kataka kutuzunguka kwa njia ya matendo kamili ya kibadamu kupitia Mwanae na hivyo Baba alipenda kuunda kwa upya matendo yetu ili yaweze kufanana na Kristo na ili tuweze kutimiza matendo mema ambayo Mungu ameandaa ili tutembee ndani mwake (Ef 2,10).

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

01/03/2018 16:29