2018-02-28 15:38:00

Papa:Altareni ndiyo Kitovu cha Msalaba na ndiyo Yesu mwenyewe!


“Tuendelee na katekesi juu ya Misa takatifu: Katika Liturujia ya Neno, niliyoelezea siku silizopita katika kateksi, inafuatia sehemu nyingine ya Misa ambayo ni Liturujia ya Ekaristi. Kwa upande wake katika ishara Takatifu, Kanisa linaendelea kuwapo katika Sadaka ya agano lililowekwa muhuri na Yesu katika altare ya Msalaba” (taz CONC. ECUM. VAT. II, Cost. Sacrosanctum Concilium, 47).

 Ni utangulizi wa tafakari ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko alio anza nao, wakati wa katekesi yake ya kila Jumatano, ambapo tarehe 28 Februari 2018 kwa mwendelezo wa tafakari juu ya misa, amejikita katika liturujia ya Ekaristi. Na  Kabla ya kuanza takafakari, Imesomwa Injili ya Marko: “Yesu aliwauliza ; Je kuna mikate mingapi? Nendeni mkatazame, mitume wakamjibu; ni nikate mitano na samaki wawili.Bwana akawaagiza wakae wote(…)Alichukua mikate mitano na samaki wawili katazama juu na kuibariki, akauma na kuwapa mitume wake ili wawagaiwie”(…)( taz Mako 6,38-39.41).
 
Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anasisitiza kuwa  altare ya Msalaba ndiyo ilikuwa ya kwanza  ya kikristo, sisi tunapokaribia altareni kuadhimisha Misa, ni kumbukumbu yetu ya altare ya Msalaba mahali ambapo ilifanyika sadaka ya kwanza.  Kuhani katika Misa, anawakilisha Kristo na kutimiza ambacho Bwana mwenyewe alifanya, na kuwakabidhi mitume wake wakati wa karamu ya mwisho: alichukua mkate na kikombe, akashukuru na kuwapa mitume wake akisema, “Twaeni mle na kunyweni: huo ndiyo mwili wangu na damu yangu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Kwa utii wa amri ya Yesu, Kanisa limeweka Liturujia ya Ekaristi katika kipindi kiendacho na maneno na ishara alizofanya Yeye wakati wa mkesha wa mateso yake. Kwa namna hiyo katika kuandaa zawadi, zinapelekwa altareni mkate na divai, ikiwa na maana ya vitu viwili ambavyo Yesu alivishika mkononi mwake.

Katika sala ya ekaristi tunamshukuru Mungu kwa matendo ya ukombozi na sadaka iliyogeuka mwili na damu ya Yesu Kristo. Baadaya inafuata kuumega mkate na kumunio, mahali ambapo  wote tunafanya uzoefu wa Mmitume ambao walipokea zawadi ya ekaristi kutoka mikono ya Yesu mwenyewe.(taz Misale ya Roma 72)

Baba Mtakatifu akendelea kueleza ishara ya kwanza ya Yesu, “ alichukua mkate na kikombe cha divai, vitu viwili vinaendana na maadalizi ya vipajii. Ndiyo sehemu ya kwanza ya Liturujia ya ekaristi. Ni vema waamini kuwakilisha kwa Padre mkate na divai ina maana ya sadaka ya kiroho ya  Kanisa kupokelewa katika Ekaristi. Na hivyo Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa ni vizuri waamini ndiyo wapeleke vipaji vya mkate na divai mbele ya altare.

 Pamoja na hayo anafafanua kuwa hata kama leo hii waamini hawapeleki vipaji hivyo kama ilivyokuwa mwanzo, mkate na divai kwa ajili ya Liturujia, bado lakini uwakilishwaji wa vipaji hivyo unabaki na thamani na maana hiyo kiroho ((ibid., 73). Ina maana kwa kawaida katika utoaji wa daraja la upadre, wakati Askofu akikabidhi mkate na divai: anasema pokea sadaka ya watu watakatifu kwa ajili ya sadaka ya ekaristi.

Watu wa Mungu wanapopeleka vipaji, mkate na divai, ni sadaka kubwa kwa ajili ya misa kwa maana hiyo, ishara ya mkate na divai inayopelekwa mbele na waamini katika mikono ya padre, ambaye baadaye anaiweka juu ya altare kitovu cha Liturujia nzima ya Ekaristi. Kwa maana hiyo kitovu cha Misa ni Altare na altare ni Kristo; ni lazima kutazama daima altare ambayo ni kitovu cha Misa.

Tunda la kazi ya mikono ya binadamu inapelekwa kama ishara ya  uwajibikaji  wa waamini kwa kutii Neno la Mungu  ambayo ni sadaka inayokubaliwa na Mungu mwenyezi, kwa ajili ya wema wa Kanisa lote takatifu. Na namna hiyo maisha ya waamini katika mateso, sala zao  na kazi zao, zinaungana na sadaka na mateso kamili ya Kristo ambapo kwa mtindo huo unapata thamani mpya (taz KKK 1368).

Ndiyo sadaka yetu, kwa hakika ni ndogo, anathibitisha Baba Mtakatifu, lakini Kristo anahitaji kidogo hicho. Yeye anaomba kidogo lakini anatupatia kiasi kikubwa; katika maisha yetu ya kawaida  yakuwa na  na mapemzi mema, Bwana anataka mioyo iliyo wazi, anataka tuwe bora ili kupokea kutoka kwake yeye anayejitoa sadaka mwenyewe katika Ekaristi; yeye anaomba ishara hizi wazi ambazo baadaye zinageuka kuwa mwili na damu yake.

Sura hiyo katika mchakato mzima wa sala hiyo unawakilishwa na uchomaji wa ubani kwa moto, moshi utandao mpaka juu, na kufukia sadaka kama wafanyavyo katika sikukuu, kufukizia msalaba, altare, padre  na watu kuonesha wazi ule mpango wa sadaka inayowakilisha kuunganisha hali halisi hiyo ya sadaka ya Kristo. 

Baba Mtakatifu maezidi kuhimiza kuwa, wasisahau kuwa kuna Altare ambayo ni Kristo lakini daima inayojieleza hawali ya yote kuwa, altare ya kwanza ni Msalaba, juu ya altare ambaye ni Kristo tunapeleka vipaji vyetu vidogo , mkate na divai, ambayeo baadaye nitageuka kuwa Yesu Kristo anayejitoa kwa ajili yetu.

Hiyo yote ikiwa inajieleza hata katika maombi juu ya sadaka. Katika maombi hayo Padre anaomba Mungu apokee sadaka ya Kanisa inayotolewa , akiomba tunda la kudilishana kutoka katika umaskini wetu na utajiri wake. Katika mkate na divai tunawakilisha sadaka ye maisha yetu ili kuyabidili kwa Roho Mtakatifu katika Sadaka ya Kristo na kwake yeye iguzwe  kuwa sadaka ya kiroho inayompendeza Baba. Wakati wa kumaliza mandalizi ya vijaji, ni kujiweka tayari katika maombi ya Ekaristi.

Baba Mtakatifu amemalizia katekesi yake akieleza kuwa, tasaufi ya kujitoa binafsi  katika kipindi hicho cha misa inatufundisha na inaweza kutuangazia siku zetu kuwa na  uhusiano mwema na wengine, mambo tufanyayo, mateso tunayokutana nayo, kwa kusaidiwa kujenga mji mwema kwa mwanga wa Injili. 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.