Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Wazee na wagonjwa ni makaa ya moto ya ushuhuda,imani na matumaini!

Wazee na wagonjwa ni makaa ya moto ya ushuhuda,imani na matumaini!

27/02/2018 09:01

Baba Mtakatifu wakati wa ziara yake fupi ya kitume katika Parokia ya Mtakatifu Gelasio I, amekutana na wazee na wagonjwa wa parokia hiyo katika ukumbi wa maonesho ya Parokia. Katika kuwasalimia na kuzungumza nao bila maandishi anawashukuru kwa yote wanayotenda kwa ajili ya ulimwengu na kwa Kanisa.

Lakini pia anasema, labda mwingine anaweza kusema je mimi ninafanya kitu gani kwa ajili ya ulimwengu? Siendi katika Umoja wa Mataifa; katika mikutano,bali niko nyumbani …. Ninafanya nini kwa ajili ya Kanisa? Kanisa ndilo linafanya kwa ajili yangu… Hapana Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, ushuhuda wa kila mmoja wao  wa imani, upendo kwa watu, kutia moyo wengine  ni kama vile makaa ya kutunza moto ndani ya majivu. 
Wao  ni makaa ya moto, makaa ya ulimwengu,yaliyopo katikakati ya majivu: chini ya matatizo, chini ya vita kuna makaa ya moto , makaa ya imani , makaa ya matumaini  na makaa ya furaha iliyofichika.

Baba Mtakatifu anaowaomba waendelee kutunza makaa ya moto hayo waliyo nayo ndani ya mioyo yao na ushuhuda wao.  Katika matatizo yaliyopo na yale yatakayokuja, lakini wakiwa na utambuzi kuwa, wao ni wamisionari  katika dunia na kwa Kanisa. Waendelee mbele na moto uliofichika ndani ya  maisha. Kwasababu kuishi kwao si bure ni moto ambao unotoa joto  na umefanya mambo mengi.

Mwisho wake moto ukizimika, yanabaki, makaa. Na hivyo wao wasisahau kuwa ni makaa ya ulimwengu na ya Kanisa kwa ajili ya kupeleka moto mbele. Waongee na vijana, wawasililize vijana, kwa maana vijana wanahitaji! Wasikaripie vijana, bali waache waongee na kuuliza maswali ya mambo mengi ambayo yapo katika akili zao, kwa maana si rahisi kuwatambua vijana.

Lakini kwa njia ya kuzungumza kwa maana wanahitaji kusikia uzoefu wao , wanayo haja ya moto uliojificha ambao huko ndani ya makaa yao. Baba Mtakatifu kwa urahisi wa lugha yake amezidi kusisitiza ya kuwa, wasisahau kuwa wao ni makaa ya moto wa Yesu, wa historia, ya ulimwengu na Kanisa. Wao ni makaa chini ya majivu! 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

 

27/02/2018 09:01