2018-02-27 14:00:00

Papa:Bwana hachoki kuita kila mmoja abadili maisha na kuongoka!


“Bwana hachoki kuita kila mmoja ili abadilishe maisha na kufanya hatua ya kwenda kwake kwa ajili ya kuongoka. Anafanya hivyo kwa ukarimu na imani kama Baba kwa njia hiyo, hata sisi tufanye hivyo katika maungamo. Ni ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake tarehe 27 Februari 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta. Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema, kwaresima ni kipindi kinachosaidia uongofu, ili kumkaribia Mungu kwa ajili ya mabadiliko ya maisha yetu na hiyo ni neema ya kuomba Bwana, kwa maana Bwana anaita kwa ukarimu na matumaini kama Baba!
 Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha maneno  hayo kutokana na somo la siku la Nabii Isaya, anayealika uongofu wa kweli, anasisitiza kwa kuonesha tabia maalumu ya Yesu mbele ya dhambi zetu. 

Yeye hatishii, bali  anatoa wito kwa ukarimu na kutupatia matumaini akisema “ haya njoni tumesemezane”,kama  maneno ya Bwana aliyowalekeza wakuu  wa Sodoma na watu wa Gomora, ambao anataka waondoe uovu na matendo yao mabaya machoni pake (taz Isa 1:10,15-20)! “Haya njoni tumezane asema Bwana, Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. Kwa maana hiyo Baba Mna ni kama baba na kijana ambaye amefanya ukorofi, anapaswa kukaripiwa. Lakini mtoto huyo anatambua kuwa akienda na fimbo, mambo yatakuwa mabaya, hivyo lazima aende kwa imani.

Katika sehemu hii Baba Mtakatifu anafafanua kuwa la Neno Bwana linatualika hivi: njoni tukanywa kahawa pamoja na tusemezane.Usiwe na hofu, sitaki kukupiga kiboko. Kwa maana anajua jinsi gani mtoto anafikiri kama tabia za kitoto: “mimi sijafanya lolote kwa haraka”. Lakini Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Kama baba mbele ya mtoto wake kijana, ndivyo Yesu anataka kufanya ishara ya matumaini kila anayekaribia kitubio na kubadili moyo. Aidha Baba Mtakatifu akikumbuka uongofu wa Zakayo au matayo mtoza ushuru, anasema, ndivyo anataka hata katika maisha yetu. Yesu anataka tujikite katika hatua mbele ya uongofu.

Tumshukuru kwa wema wake. Yeye hataki kutupiga kiboko na kutuhukumu. Yeye alitoa maisha kwa ajili yetu na ndiyo wema wake. Yeye daima anatafuta njia ya kuweza kufikia moyo wetu. Kama Makuhani ambao wamepewa nafasi ya Bwana, lazima kuhisi uongofu, hata wao wawe na tabia za wema kama asemavyo Bwana: “njoni tusemezane, hakuna shida, msamaha upo na si kutishia tangu mwanzo”. Baba Mtakatifu ametoa mfano wa uzoefu wa Kardinali mmoja muungamishi ambaye alisema kuwa, mbele dhambi ambayo ni kubwa hakai muda mrefu, bali ni kuendelea mbele katika mazungumzo. Kutokana na hilo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, hiyo inasidia kufungua moyo, kwasababu mtu huyo uhisi amani . Na Bwana anafanya hivyo akisema, njoni tusemezane na kuzungumza! Chukua listi ya msamaha, kwa maana msamaha upo!

Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu, hii inamsaidia kuona tabia ya Bwana ya kwamba ni kama Baba na mwanae anaye amini kuwa amekua wakati huo yuko nusa ya safari, Bwana anatambua kuwa sisi sote tuko nusu ya safari  na mara nyingi tunahitaji kusikiliza neno hilo, “njoni  na msogope njoni na msamaha upo”. Tabia hiyo inatia moyo wa kwenda kwa Bwana kwa moyo ulio wazi, kwa maana ni Baba anayesubiri!

Sr Angela Rwezaula

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.