Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Yesu alitangulia kuwaonesha mitume wake jinsi gani anaishi huko mbinguni!

Akiwa katika ziara ya ya parokia ya Mtakatifu Gelasio mjini Roma Tarehe 25 Februari 2018 amewaalika waamini kusikiliza sauti ya Bwana

26/02/2018 15:13

Jumapili 25 Februari 2018 Baba Mtakatifu Francisko alifanya ziara yake fupi katika Parokia ya Mtakatifu Gelasio I nje kidogo ya mji wa Roma. Wakati wa mahubiri yake anasema; Yesu anajionesha kwa mitume wake jinsi alivyo huko mbinguni, anayeng’aa, anatukuka  na mshindi. Anafanya hivyo ili mitume wake waweze kukabiliana na mateso , kashfa ya msalaba, kwa maana wao walikuwa hawajuhi kwamba Yesu anatakufa kama muhalifu, hilo  wasingetambua! Anathibitisha.

Walikuwa wanajua  kuwa Yesu ni mtawala na ukombozi wa dunia hii  kama vile wale watawala ambao wanashinda daima katika mapigano ya vita. Lakini njia ya Yesu  ni nyingine; ushindi wa Yesu ni kwa njia ya unyenyekevu katika msalaba.  Na kutokana na kwamba jambo hilo lingeonekana la kashfa kwao, Yesu anaamua kuwaonesha ni jambo gani hasa  litatokea mara baada ya tukio hilo; ni kitu gani kitawadi  baada ya msalaba, lakini pia ni jambo gani tunasubiri hata sisi sote!

Ni utukufu na mbingu hiyo. Ndilo jambo zuri, kwasababu Yesu daima anatuandaa kwa njia ya majaribu. Kwa namna moja au nyingine lakini ndiyo ujumbe ya kwamba daima anatuandaa. Anatupatia nguvu za kwenda mbele wakati wa majaribu na kuyashinda kwa nguvu zake. Yesu hatuachi kamwe peke yetu katika majaribu ya maisha. Anatuandaa na kutusaidia kama alivyo wandaa mitume wake katika maonesho ya utukufu. Kufanya hivyo mitume watakumbuka kuchukua msalaba kwa unyenyekevu. Jambo la kwanza la mafundiho ya  Kanisa ni kwamba Yesu anatuandaa daima katika majaribu yanayoendelea na hatuachi peke yetu kamwe!
 
Jambo la pili ambapo lazima kutambuliwa katika Neno la Mungu, Baba Takatifu Francisko anasema; “Tazama huyo ndiye mwanangu mpendwa, msikilizeni yeye”. Huo ni ujumbe ambao Baba wa mbinguni awanawapatia mitume wake. Ujumbe wa Yesu ni kuwaandaa kwa kutazama utukufu wake; ujumbe wa Baba wa mbinguni unasema“ msikilizeni Yeye. Hakuna kipindi chochote cha maisha yetu ambacho unaweza kuishi kwa ukamilfu, iwapo husikilizi Yesu. Baba Mtakatifu anabainisha: Wakati mzuri simama na sikiliza Yesu; wakati mbaya simama na  sikiliza Yesu. Hiyo ndiyo njia! Yeye daima ataelekeza nini la kifanya d. Tuendelee mbele katika kipindi hiki cha kwaresima kwa mambo mawili: katika majaribu , kukumbuka utukufu wa Yesu, yaani kile ambacho kinatusubiri. Yesu yupo daima na utukufu wake kutupatia nguvu . Na kipindi chote cha maisha , sikiliza Yesu anasema nini. Ni katika Injili, katika Liturujia , daima Yesu anaongea katika mioyo yetu.

Katika maisha yetu ya kila siku labda kuna matatizo au mambo mengi ya kutatua. Lakini vema kutafakari je Yesu anataka kusema nini leo? Jaribu kusikiliza sauti ya Yesu anasema nini ndani ya dhamiri ya moyo. Na kwa njia hiyo ni kufuata ushauri wa Baba yake kuwa “ huyu ndiyo mwanangu mpendwa , msikilizeni Yeye. Atakuwa mama Maria ambaye kwa mujibu wa ushauri wake  huko Kana ya Galilaya aliweza kufanya miujiza ya maji kuwa divai. Maria aliwaeleza nini wafuasi wake? “fanyeni atakalowambia. Kwa maana ya kusikiliza Yesu na kufanya kile ambcho anasema, ndiyo njia ya uhakika. Ni kwenda mbele na kumbukumbu ya utukufu wa Yesu na ushauri huo wa kusikiliza na kufanya kile ambacho anasema.

 
Sr Angela Rwezaula
Vatican News

26/02/2018 15:13