Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Mahubiri

Msihukumu badala yake ni kuomba msamaha na neema ya kuona aibu!

Wito wa Baba Mtakatifu kwa waamini kukumbuka hukumu tuliyo nayo mbele ya Mungu!

26/02/2018 14:57

Msihukumu msije nanyi  hukumiwa ni wito wa Injili ya siku ambao Baba Mtakatifu Francisko ameufafanua kwa kina katika mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, asubuhi ya tarehe 26 Februari 2018. Badala ya kuhukumu, Baba Mtakatifu anawaalika waumini wote kusamehe jirani na kuomba neema ya kuona aibu binafsi .

Akitafakari kwa kina juu ya Injili ya Siku kutoka Mtakatifu (Lk 6,36-38),anasema kuwa, katika kipindi cha kwaresima, Kanisa lote linaalikwa kujiangalia kwa upya, kwa maana hakuna hata mmoja atakayeweza  kukwepa hukumu ya Mungu, yaani ile binafsi na ya dunia, kwa maana wote kwa dhati tunahukumiwa. Kwa mtazamo huo Kanisa linatafakari zaidi hasa kwa tabia tulizo nazo dhidi ya jirani na Mungu.

Baba Mtakatifu anasema, kila mtu anaweza kufikiria na kutafiti  dhamiri binafsi, je inewahi kuhukumu au ninajifanya hakimu. Hali kadhaliaka ni lazima kutazama mazungumzo yetu ambayo daima hukukumu wengine. Lakini je Baba Mtakatifu anauliza kwa nini unajifanya hakimu wa wengine ? Kuhukumu wengine ni jambo baya , kwasabu hakimu ni mmoja naye ni Bwana anayetambua tabia ya binadamu!

Kwa kuzingatia hayo zaidi, ametoa maswali kwa mifao: katika mikutano yetu, wakati wa chakula au kila chochote tufanyacho kwa , masaa  mawili ya kukutana ni dakika ngapi tumehukumu wengine? Ni lazima kuwa na huruma kama alivyo Baba Yetu wa mbinguni na  lazima kuwa wakarimu. Toeni , nanyi mtapokea, je ni kitu gani tutapewa? Ni kile kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu” kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa” kama isemavyo Injili ya Bwana anathibitisha Baba Mtakatifu Francisko!

Kwa njia hiyo wito ni ule wa kuwa na huruma kwa wengine kama vile Bwana anavyokuwa na huruma kwetu. Akiendela na takafakri la pili Baba Mtakatifu anasema ujumbe wa Kanisa leo  hii unatoa mwaliko wa kuwa na tabia ya unyenyekevu  na Mungu ambaye anasisitiza juu ya kujitambua dhambi binafsi. Sisi tunatambua ya kuwa haki ya Mungu ni huruma, lakini lazima kusema na kukiri binafsi kumwamini Bwana mwenye haki na huruma, na kuwa na aibu mbele ya Mungu kwa kumtendea dhambi.

Mwisho Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa, katika lugha yake ya kuzaliwa, mtu akitenda yaliyo mabaya mbele ya watu, mama anakemea kuwa, jionee aibu na kumwambia aombe msamaha haraka ili wasiwe na haibu mbele ya Mungu!
Ni neema sana ya kuwa na aibu, anakumbusha Baba Mtakatifu na hivyo tabia hizo mbele ya jirani ni kutaka kukumbusha kuwa, kipimo kile kile mpimacho cha kuhukumu ndicho mtakachopimiwa wakati wa kuhukumu.
Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

26/02/2018 14:57