Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maisha Ya Kanisa Afrika

Padre Zagore:Ni vema kushinda dhambi ya ukabila,si tabia ya kikristo!

Tukio lililotokea katika Jimbo la Ihara nchini Nigeria litufundishe wakristo kushinda dhambi ya kuwa na ukabila - REUTERS

24/02/2018 09:33

Jambo lililo jitokeza  la ukabila hadi kufikia hatua yake kujiudhuru  ni suala ambao limetoa mwangwi sana katika Makanisa ya Afrika. Hayo ni maneno kwa mujibu wa mmisionari Mtaalimugu wa Nigeria Padre Zagore akithibitsha kuwa ni lazima kushinda dhambi ya ukabila. Askofu Peter Ebere Opkalaeke tangu kuteuliwa kwake 2012 hakupokelewa vema  na watu wa ardhi yake, hadi kufikia hatua ya kuomba kustaafu. 

Kwa maana hiyo kipeo cha jimbo la Ihara ni kama mlima wa theruji uliochomoza matukio yenye mzizi ya dhambi na hatari ya ukabila kwa mujibu wa mtaalimugu Padre  Donald Zagore kutoka  nchi ya Ivory Coast,ambaye ni mmisionari wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (SMA) wakati wa mahojiano yao na Shirika katoliki la habari Fides.

Padre Zagore anaendelea kueleza  kuwa iwapo ndani ya Kanisa katoliki  mahali ambapo panafikiriwa kuwa kundi moja la ukristo penye umoja, undugu na muungano wa watu, panaleta mgawanyiko  kutokana na masuala ya ukabila na ukoo, lazima kujiuliza maswali ya kinabii; je tumeelewa maana ya wakati wetu na imani yetu? Kwa bahati mbaya anaendelea, hayo yanakuja kutambuliwa  siku hadi  siku kuwa, damu ya utamaduni,kabila na ukoo bado zinabaki kuwa na nguvu na  muhimu  zaidi kuliko maji matakatifu ya ubatizo kwasababu ya matukio yaliyojionesha.

Kutokana na hilo,dhana ya Kanisa kama familia ya Mungu Afrika wakati mwingine utafikiri inakosa mwelekeo wa mazungumzo kwa maana ya kuonekana sura zenye mantiki ya uongo. Utakuta mara wanasogea zaidi katika familia ya Kanisa ya Mungu ndani ya Kanisa la ukabila. Kwasababu ya matukio hayo ni lazima kusema wazi kwa nguvu zote kuwa, tabia za namna hiyo si za kikristo.

Kwa mujibu wa Padre Zagore anasema, ukabila kwa hali zozote hauna tabia ya Kanisa la Yesu Kristo. Ni thamani mojawapo kubwa inayobaki ya shauku ya kutumikia Mungu chini ya mapenzi yake; mapenzi yake yanayotokana na upendo upeo na kuishi kwa pamoja. Kama Kristo, lazima kwa njia zozote kukataa kufungwa minyororo ya ukabila na ukoo; ni lazima kuwa wazi na kufunguka kwa kila binadamu kuanzia asili ya utamaduni, rangi na kabila. 

Kama Mtakatifu Paulo Mtume wa watu anavyosema katika jumuiya kuwa katika Kristo hakuna myahudi, wala mgiriki ; hakuna mtumwa na huru ; hakuna mwanaume au mke  kwa maana wote ni wa Kristo Yesu (Gal 3:28). Hiyo ndiyo dharura msingi ya kazi ya kichungaji katika Kanisa hasa la Afrika ili kueza kushinda dhambi ya ukabila na ukoo kwa maana si tabia ya Kanisa la Kristo, amehitimisha Padre Zagore!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 

24/02/2018 09:33