2018-02-24 10:05:00

Kazi kuu ya uekumene ni kutembea hatua kwa hatua pamoja kuelekea umoja!


Sisi ni kitu kimoja pamoja na tofauti zetu tulizo nazo na si wengi wanaotafuta kuwa wamoja. Ndiyo tunaitwa Kanisa la wasio kuwa na mwisho na ndiyo hiyo  changamoto ya uekumene ambao Makanisa ya milenia ya tatu wanakabiliana nayo. Haya ni maneno ya askofu Mkuu Justin Welby wa Canterbury Uingereza na Mkuu wa Shirikisho la Kianglikani akitoa tafakari yake katika moja ya mfululizo wa mikutano huko Geneva  hivi karibuni, ulioandaliwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc) kwa ajili ya kuadhimisha mwaka wa 60 tangu kuanza kwa chombo hiki.

Maadhimisho ya kumbukumbu leo hii ni kama fursa kwa ajili ya hatua nzima za kiekuemene ili kuweza kutembea pamoja kupitia  hatua zilizofanyika wakati uliopita na kuwa na mtazamo wa hatua  endelevu ya kutambua jinsi gani kwa pamoja Makanisa yanaweza kujikita mbele ya changamoto hizi za dunia kwa ajili ya amani na mapatano.

Mazungumzo ya taalimungu yamepelekea matunda makubwa anathibitisha askofu Mkuu Welby katika hotuba yake. Katika karne ya 20, wameweza kuwa na  ukaribu muhimu wa taalimungu na mafundisho kati ya Makanisa. Ni miaka 22 karibu imepita  tangu alipongea kuhusu vuli la  Uekumene  kwa mara ya kwanza katika Mkutano huo  akiwa kama Katibu Mkuu. Licha ya hayo vuli hilo lilitambuliwa kwa kutoa  matunda muhimu, makubaliano ya kiteolojia ambayo hadi sasa yanapiga hatua kwa hatua katika makanisa kuelekea umoja. Aidha anasema kuwa utajiri wa matokeo ya kiekumene yamempa msukumo Kardinali Walter Kasper kuandika kitabu kisemacho “uvunaji wa  matunda”.

Askofu Mkuu Welby anatoa  ufafanuazi kuwa, mengi hata kama si yote , mgawanyiko wa Kanisa unatazama masuala  msingi na mafundisho, masuala ya utawala na madaraka hata kama siyo migongano ya mipaka. Ni masuala ambayo yalitokeza kuta ambazo zilitoa kizuizi katika maeneo na kujileza uzalendo.  Mipaka ambayo inaonesha utofaui , kwa upande mwingine anasema ni mtu, na upande mwingine ni utamaduni, kabila nyingine na taifa jingine. Yote haya yanahitaji utambuzi , kama Makanisa yanavyotaka kuishi mipaka hiyo kama nafasi zilizofungwa  au milango iliyofunguliwa.

Mipaka iliyofunguliwa  Askofu Mkuu anafafanua  kuwa, inawezesha kuwa nafasi ya kuingia mwingine na  kufanya kuwa sehemu yetu. Inawezesha kuwa  hata  mwendo ambao siwa kugawanya na wala kuwa na utofauti, bali  kufunguliwa kwake kuwa wazi katika makutano. Kwa kutazama mbele ya upeo huo anaona kuwa, upo uekuemene wa matendo ya taalimungu, akikumbuka hata mkataba wa pamoja uliosainiwa na Papa Francisko wakati wa tukio la jubilei ya miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na Askofu Mkuu wa Kianglikani Michael Ramsay.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Welby anasema uekeumene wa matendo unashuhudia  kuwa mbele ya mabaya, wakristo wote  wanaungana katika upendo na kuonesha umoja. Aliyasema hayo hayo muhubiri mkuu wa  nyumba ya Papa, Padre Raniero Cantalamessa mwaka 2015, mbele ya Malkia Elizabeth  katika Kanisa Kuu la Westminster Uingereza. Alishuhudia maneno hayo kwamba, "wanapotaka kuua hawaulizi kama ni wakatoliki, waorthodox , wapentekoste au waanglikani, bali wanauliza kama ni wakristo"!

Mwisho Askofu Mkuu  wa Shirikisho la Kianglikani amekumbisha siku za mwanzo wa uchgauzi wa Papa Francisko, wakati akihutubia  makleri na wachungaji kuwa " wanapaswa kuwa na harufu ya wachungaji , kwenda katika zizi"(kwa maana hiyo katika mipaka ili kutafuta hasa zaidi aliye baki nje). Anaihitimisha:hiyo ndiyo kazi kubwa lakini ikiwa na maana ya uwajibikaji kwa makanisa yote kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kutafuta aliyepotea mahali popote alipo. Ni kwa sababu ya kutaka kugundua kuwa zizi ni moja kama alivyo mchungaji mwema anayesali ili sisi wote tuwe na umoja

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.